Hofu imetanda
katika mji wa Kasulu kufuatia vurugu zinazofanywa na madreva pikipiki maarufu
kama Bodaboda ambao wanafanya maandamano kuelekea kituo cha polisi kushinikiza
wenzao wanaoshikiliwa waachiwe huru.
Hali hiyo
imeanza majira ya saa sita mchana baada ya kile wanachodai kuwa askari wa
usalama barabarani tangu asubuhi wamekuwa wakikamata bodaboda na kasha kuwapiga
bila makosa.
Barabara kuu
ya mjini Kasulu itokayo maeneo ya makaburini hadi kituo cha polisi imefurika
pikipiki zinazoendeshwa kwa fujo kuelekea mtaa wa mlimani kwa ajili ya
kushinikiza polisi kuwaachia wenzao waliokamatwa
Hata hivyo
habari zinaeleza kuwa, mtu mmoja leo amegongwa nagari eneo la soko kuu kutokana
na kile kinachoelezwa kuwa ni msongamano wa pikipiki zinazopaki katika makutano
ya barabara hali inayosababisha upishanaji wa watembea kwa miguu, magari na
pikipiki kuwa wa shida.
Mzee huyo
ambaye jina lake hadi sasa halijajulikana amelazwa katika hospitali ya wilaya
ya Kasulu.