Watu 36 wamefariki dunia
katika ajali ya magari mawili ya abiria wilayani Butiama mkoani mara mapema leo
Habari kutoka kwa jeshi la
polisi mkoani Mara zinasema kuwa ajali
hiyo imehusisha mabasi ya kampuni ya Mwanza Coach na J4 yanayofanya safari
kutoka Butiama kwenda Mwanza
Imeelezwa kuwa ajali hiyo
imetokea leo asubuhi katika eneo la sabasaba ambapo watu wengine 79
wamejeruhiwa na wanapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Butiama
Jeshi la polisi linafanya
uchunguzi zaidi kuhusu chanzo cha ajali hiyo