Na Emanuel Michael, Kigoma.
MWANAFUNZI wa darasa la saba miaka 14 amebakwa mapema wiki
hii kabla ya kuanza mtihani wa kumaliza elimu ya msingi katika kijiji cha
Bukuba, Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma.
Akizungumza na waandishi wa habari, Bi. Anisia Enock ambaye
ni mama wa mtoto huyo, alisema kuwa mtoto wake alibakwa na Amoni Samwel (25) mkazi
wa Mwanga B na kuhatarishiwa hatimayake ya kufanya mtihani.
Alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 12 jioni wakati
mwanye huyo alipokuwa akielekea dukani kuchukua simu, mbani ndipo wazazi
walipohoji uchelewaji huo na mwanaye akaeleza alichotendewa na Amoni Samwel.
“Binti yangu aliponisimulia nilichanganyikiwa kwani
anatarajiwa kufanya mtihani Jumatano na nilipomchunguza
alikuwa akitokwa na damu zilizotapakaa
kwenye makalio ndipo nikaamua kumpigia simu baba yake kabla ya kwenda kwenye vyombo vya sheria”
alisema Bi. Enock.
Aidha Enock alisema kuwa alienda kutoa taarifa polisi na
baada ya kuandika mashtaka alipewa PF3 kwaajiri ya kwenda Hospitali na walipofika binti yake akafanyiwa
vipimo sambamba na kupatiwa matibabu.
“Siku ya jumatatu Maafisa usitawi wa Jamii walifika na
kumfanyia vipimo upya na kumpatia dawa tena ili kumpa nguvu ya kufanya mtihani”
aliongeza
Kwa upande wa mwanafunzi aliyebakwa jina linahifadhiwa, alisema kuwa baada ya kutumwa na mama yake
alikutana na mwanafunzi mwenzake wa kiume na kumuomba amuelekeze
walichofundishwa darasani na ndipo Amoni Samweli alipowakuta.
Aliongeza kuwa baada Mbakaji kuja aliwauliza walichokuwa
wanafanya, nao wakamjibu kuwa wanasoma
lakini yeye akakataa na kuanza kumpiga makofi yule mvulana sanjari na kumwambia
aondoke eneo mlile.
“Baada ya kumfukuza mwanafunzi mwenzangu alinambia nivue
nguo mimi nikakataa ndipo akanibeba na kunipeleka kwenye shamba la ndizi na kunifumba
mdomo ili nisipige kelele huku akinitishia kunichoma kisu hapo ndipo akanibaka”
aliongeza.
Nae Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Buhigwe, Godfrey
Kapaya alisema kuwa walifika nyumbani kwa mwanafunzi huyo na kumfanyia vipimo
vilivyothibitisha tukio hilo na alikuwa na maumivu sehemu za siri.
“Baada ya hapo tulimpa dawa za maumivu, dawa za kuzuia
maambukizi ya magonjwa ya zinaa pamoja na mimba” alisema Kapaya.
Kapaya aliongeza kuwa kwakuwa mwanafunzi alitakiwa kuingia
kwenye mtihani walimpa ushauri wa kumuondolea
hofu ili afanye mtihani akiwa katika
hari nzuri ya kimawazo.
Pamoja na hayo Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma, Japhari
Muhamed alithibitisha tukio hilo na kuongeza kuwa mtuhumiwa tayari yuko
mahabusu na hatua za kumfikisha mahakamani zinaendelea.
“Kitendo hiki ni kibaya sana na sisi tunakilaani kwani ndio
tunaolinda watoto na wananchi kwa ujumla sasa ili iwe fundisho kwa wengine
lazima mtuhumiwa ahukumiwe” alisema Muhamed.
Muhamed aliwataka wananchi kuwawaelimishe watoto wao
wasitembee sehemu zisizo salama wakiwa peke yao hasa mida ya usiku pia na
wazazi wawe makini kuwaacha watoto zao peke yao sambamba na kutoa taarifa pindi
wanaposikia matukio kama haya.
Mwisho.