Watu watano majambazi wanaodhaniwa
kuwa Raia wa Burundi wameuawawa katika majibizano ya risasi na askari Polisi
wilayani Kasulu
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma ACP Jafary Muhamed amesema
kuwa tukio hilo limetokea leo asubuhi katika eneo la Maragalasi na kwamba
walikuwa katika jaribio la kuteka mabasi yanayofanya safari zake kati ya
Kigoma, Dar es Salaam, Kahama na Mwanza.
Watatu kati ya waliouwawa walikuwa wamevaa sare za kijeshi
ambazo zinadhaniwa kuwa ni sare za jeshi la Burundi.
katika tukio hilo, Bunduki mbili
aina ya SMG, risasi 65za SMG na mabomu matatu ya kutupwa kwa mkono yamekamatwa
Polisi
wanaendelea na msako katika porii la Maragalasi ili kubaini kama kuwa kambi
inayotumika kuhifadhi silaha
Vijiji vinavyopakana
na pori la Maragalasi hususani Mvugwe na Busunzu vimekuwa vikikubwa na matukio
mengi ya uvamizi na uporaji unaohusisha silaha za kivita
Inaelezwa kuwa
matukio hayo yanawahusisha watanzania wanaoshirikiana na Raia wa Burundi
Mwezi uliopita
watu watano abiria waliokuwa wakisafiri kutoka vijiji vya mpakani mwa Tanzania na
Burundi walipoteza maisha baada ya gari lao kutekwa na kasha kutupiwa bomu la
kutupwa kwa mkono