HAYATI IDD AMINI DADA |
Alikuwa mwanajeshi mahili aliyekuwa na
uwezo mkubwa wa kijeshi pamoja na elimu ndogo aliyokuwa nayo.
Utawala wa Uingereza ulimuingiza
katika jeshi la afrika mashariki kabla ya Uhuru na aliwahi kutumikia jeshi hilo
nchini Barma, kutokana na maguvu alikuwa bondia aliyepata umaarufu na hivyo akapanda
haraka ngazi za kisheshi na kuwa jenerali na mkuu wa jeshi la Uganda.
Mwaka 1971 alimpindua rais Milton
Obote akajitangaza kuwa rais mpya, lakini wengine hawakumtaka.
Mara moja alianza kuwatesa wafuasi wa
Obote na watu wote waliompinga. Kuna makadirio ya kwamba jumla ya watu 100,000
hadi 500,000 waliuawa katika miaka minane ya utawala wake.
Aliharibu uchumi wa Uganda kwa ufisadi na
majaribio ya kuongoza biashara. Hatua kubwa
ya uharibifu ilikuwa kufukuza watu wote wenye asili ya Kihindi na kugawa maduka
na biashara yao kwa ndugu au wafuasi wa rais. Takriban watu 80,000 walipaswa
kuondoka kwao wakihamia Uingereza, Marekani au Canada
Pamoja na usheni huo, Iddi Amini
alikuwa na ndoto za kuhakikisha Lugha ya kiswahili inakuwa lugha kuu katika
mataifa ya Afrika Mashariki na kati, akizitaka serikali zote za Kenya, Uganda,
Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC wakati ule ikijulikana
kwa jina la ZAIRE.
Aidha Amini (Nduli) alitangaza kuwa
Uganda inaungana na Wamarekani weusi kudai uhuru dhidi ya wazungu, kupinga
Ukatili, udharirishaji na ubaguzi wa Rangi nchini Marekani (USA). Alitangaza pia
kuwa ili weusi hao wawabane vizuri wazungu ni lazima waanze kujifunza na
kutumia lugha ya Kiswahili kama lugha yao.
Mwaka 1975 alifanya mahojiano na waandishi
wa habari wa shirika la utangazaji la Ufaransa akatangaza kuwa msimamo wa
serikali yake ya kijeshi ni kuhakikisha Lugha ya Kiswahili inakuwa lugha ya
ukombozi kwa wamarekani weusi na pamoja na afrika nzima.
Alitangaza pia ndoto yake kuwa “Siku
moja wamarekani weusi wataitawala Marekani” akisisitiza kuwa waafrika wana
akili nyingi kuliko wazungu. Ndoto hii imetokea kuwa kweli baada ya Barack
Obama kushinda kuwa Rais wa kwanza mweusi marekani.
Iddi Amini alipenda sana michezo,
hususani Ngoma za asili, Soka, Masumbwi,, kuogelea pamoja na karate (angalia
picha)
Wengi hawajui kuwa IDD AMINI alikuwa
na ndoto hiyo na aliitangaza mwaka 1975. Aidha Martine Luther mmarekani mweusi
na mwana harakati naye aliwahi kutangaza kuwa na ndoto hiyo na historia
inamkumbuka yeye baada ya Obama kuwa Rais wa USA.
Pamoja na ndoto nzuri hizo za IDD
AMINI DADA (NDULI) bado hakuwa muungwana hata chembe, aliendeleza ubabe na
kukumbatia falsafa za kikatili dhidi ya raia, wanasiasa na viongozi wa Uganda,
na polepole alianza kuwa na hamu ya kuuvusha ukatili wake kwa majirani
Mnamo Oktoba 1978 Amin
alianzisha vita dhidi ya Tanzania kwa kuvamia sehemu za mkoa wa Kagera. Rais Julius Nyerere wa Tanzania aliamua
kumwondoa kwa njia ya mtutu wa bunduki na jeshi la Tanzania likatwaa Kampala mnamo
tarehe 11 Aprili 1979.
IDD Amin alitorokea Libya,
halafu Irak na mwishowe Saudia alikopewa kimbilio kwa masharti ya
kutoshughulikia siasa tena.