Rais Yoweri Museveni
ametia saini mswada wa sheria kali dhidi ya picha za ngono ambao unapinga pia
uvaaji wa mavazi yasiyo ya heshima
Sheria hiyo inatajwa
kulenga kukomesha uvaaji wa nguo nusu uchi, kwa wavulana na wasichana nchini
humo kama sehemu ya kuendelea utamaduni wa taifa hilo na wa kiafrika
Wanaotajwa kuguswa zaidi
na sheria hiyo na ngono na mavazi ni wana mitindo, wanavuziki ambao wanatajwa
kuwa vinara ya kutembea uchi hasa nyakati za maonesho ya kazi zao na wawapo
katika hafla mbalimbali za kijamii
Nguo hasa yanayovaliwa na
wanamziki na picha za watu wakiwa uchi. Mwandishi wetu wa Kampala Leylah Ndinda
na taarifa zaidi. Kusikiliza taarifa hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni
hapo chini.
Wakazi wan chi ya Uganda
wanaopenda kuvaa nguo fupi, zinazobana au zinazoonyesha sehemu za mwili ambazo
zaweza kuwafanya watu wa jinsia nyingine kusisimka na kutamani kushiriki ngono
nawe, basi jua kuwa unachungulia jela.