Na. Frida Peter
Moshi
Zaidi ya waalimu wakuu 50 katika shule za
msingi katika halmashauri za wilaya ya moshi mkoani Kilimanjaro wamevuliwa
madaraka na wengine wakihamishwa kutokana na sababu mbalimbali
ikiwemo uwezo mdogo wa utawala.
Hayo yamebainishwa na afisa elimu ya msingi wa wilaya ya Moshi
Bw. Simoni Sheshe wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua ya
serikali kutoa adhabu wa walimu hao
Bw. Sheshe amebainisha kuwa uchunguzi uliofanywa na idara ya
elimu umebaini kuwa walimu hao wamekuwa na desturi ya kujipatia kipato kinyume
cha sheria kwa kutoza fedha za vyeti kwa wanafunzi wanaohitimu darasa la saba
Sheshe amesema kuwa kufikia kwa hatua hiyo kulitokana
na malalamiko ya muda mrefu ya wazazi na wananfunzi wa shule hizo na
kwamba tume ya utumishi ya walimu na idara ya elimu imekuwa ikitoa onyo mara
kadhaa lakini walimu hao walikaidi.
Amesema waalimu wakuu hao walikuwa na tabia ya kuwatoza
kiasi cha elfu kumi kila mzazi anaye fika shuleni hapo kwaajili ya kuchukua
cheti cha darasa la saba jambo ambalo ni kinyume na utaratibu na kwamba cheti
hicho hutolewa bure bila ya malipo yoyote.