Mr. Louis Thomas - officer from International Federation for Journalists - IFJ addressing the Tanzania journalists during the seminar on crating a journalists union in Tanzania |
Dar es salaam
By. Prosper Kwigize
Waandishi wa habari nchini Tanzania wamehimizwa kuungana na
kutambua haki zao ili kujiendeleza kitaaluma na kimaslahi.
Rai hiyo imetolewa na afisa kutoka jumuiya ya kimataifa ya
waandishi wa habari IFJ Bw. Louis Thomas wakati akitoa ujumbe wa umuhimu wa
vyama vya wafanyakazi wa tasnia ya habari katika kikao cha wanahabari nchini jijini
Dar es salaam leo.
Bw. Thomas amebainisha kuwa, malipo madogo yasiyolinganga na
thamani ya taaluma katika nchini nyingi za afrika kunatokana na wanahabari
wenyewe kutotambua wajibu na haki zao katika jamii.
Amesisitiza kuwa kuundwa kwa chama cha wafanyakazi wa sekta
ya habari kutawasaidia waandishi na watumishi wa vyombo vya habari kudai na
kupata haki za msingi kulingana na weledi wao.
Hata hivyo IFJ imeonya kuwepo kwa baadhi ya waandishi wa
habari wasio na ujuzi ambao huharibu wasifu wa taaluma hiyo.