Baadhi ya boda boda zikiwa nje ya ofisi ya CCm kasulu kulalamikia unyanyasaji |
Umoja wa
vijana wa CCM wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma umemtaka mkuu wa wilaya ya Kasulu
kuitisha kikao cha kamati ya ulinzi na usalama kujadili mgogoro uliopo baina ya
jeshi la polisi na vijana waendesha bodaboda.
Rai hiyo
imetolewa na mwenyekiti wa vijana wilaya Bw. Mberwa Chidebwe katika mkutano wa
hadhara uliofanyika jana mjini Kasulu kujadili mchakato wa katiba mpya
Bw. Mberwa
ameeleza kuwa, waendesha pikipiki maarufu kama boda boda wamelalamikia kuwepo
kwa uonevu na uvunjwaji wa sheria za usalama barabarani ambao hutekelezwa na
baadhi ya askari wa jeshi la polisi
Ametaja
uonevu huo kuwa ni kukamatwa hovyo na kuombwa Rushwa, kuzushiwa kesi za uongo,
kuwekwa rumande kwa uda mrefu bila mashtaka na idara ya mahakama kuwahukumu
kifungo kinyume cha sheria za usalama barabarani
Mkuu wa
wilaya ya Kasulu Dani Makanga amekiri kupokea malalamiko hayo na kuahidi
kuchukua hatua ili kutatua mgogoro huo