|
Jet Li |
Li Lianjie (amezaliwa tar. 26 Aprili 1963) ni mshindi wa Tuzo za Filamu za Hong Kongo, akiwa kama mwigizaji bora filamu wa Kichina. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Jet Li. Jet Li ni mtaalam wa Kung Fu na Wushu. Baada ya miaka mitatu ya mafunzo ya Wushu, Jet Li alipata ushindi wake wa kwanza katika mashindano ya kitaifa ya vikosi vya Wushu kwa mji wa Beijing.
Akiwa na umri wa miaka 17, Jet Li aliachana na masuala ya Uwushu na badala yake akaja kuwa mwigizaji wa filamu na akabahatika kutoa filamu yake kwanza mnamo mwaka wa 1982 na filamu ilikwenda kwa jina la Shaolin Temple.
Badala ya hapo akawa anaendelea zaidi na maswala ya filamu na hata kuweza kujulikana katika medani hiyo ya uigizaji wa filamu katika China. Akaja kujipatia umaarufu zaidi pale alipocheza katika mfululizo wa filamu za Once Upon a Time in China, ambamo humo alikuwa akicheza kama shujaa wa kiasili - Wong Fei Hung.
Kwa upande wa Marekani, Jet Li alianza kucheza kama adui katika filamu ya Lethal Weapon 4 kunako mwaka wa 1998, na kwa upande wa filamu alizocheza Marekani kwa mara ya kwanza na kuwa kama nyota kiongozi ilikuwa katika Romeo Must Die ya mwaka wa 2000.
TANZAMA MOVIE ZAKE HAPA