![]() |
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria Kongamano la maadili lililoandaliwa na Baraza la habari Tanzania MCT mjini Bagamoyo. |
Imeelezwa kuwa maslahi duni ya wafanyakazi wa vyombo vya
habari kunatokana na kutokuwepo na chama cha wafanyakazi wa tasnia ya habari
Hayo yamebainishwa na katibu mtendaji wa Baraza la habari
Tanzania Bw. Kajubi Mukajanga wakati akihitimisha kongamano la maadili ya
uandishi wa habari mjini Bagamoyo leo.
Bw. Mukajanga amebainisha kuwa vyombo vingi vya habari haviwalipi
ipasavyo watumishi wake na huchangia uandishi wa habari zisizozingatia weledi
Aidha amepongeza kuwepo mchakato wa kuanzisha chama cha
wafanyakazi wa tasnia ya habari JUT na kuwahimiza waandishi wa habari kujiunga
ili kuwa na nguvu.