Umoja wa wazazi wilaya ya Kasulu umeazimia kuanzisha shule za awali kila kata pamoja na vyama vya akiba na mikopo kwa dhamira ya kuinua kiwango cha ufahamu wa mabadiliko ya kimaisha pamoja na kipato cha kaya na kuepuka Rushwa nyakati za uchaguzi.
Imeelezwa kuwa uwepo wa vitendo vya rushwa katika chaguzi mbalimbali kunatokana na jamii kutokuwa na elimu ya kutosha pamoja na umasikini ambao hutumiwa na wagombea kulaghai ili kupata kura
Umoja huo unaeleza kuamini kuwa endapo mfumo wa elimu za awali utaanzishwa katika ngazi cha chini pamoja na wazazi au kaya kuwa na kipato cha kutosha upo uwezekano wa wazazi kuwa na uwezo wa kupinga tabia za wanasiasa kuitumia fursa ya ujinga na umasikini kama chambo.