Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kanali mstaafu Issa Machibya |
Mkuu wa mkoa wa Kigoma kanali mstaafu Issa Machibya
amewataka viongozi wa umma kuhakikisha wanasimamia ipasavyo utekelezaji wa
ilani ya uchaguzi ili kuwaondoa wananchi katika lindi la umasikini.
Agizo hilo amelitoa wilayani Kibondo mkoni humo jana katika
ziara yake ya kukagua shughuli za maendeleo
Kanali Machibya amebainisha kuwa, kipimo cha utumishi ni
uadilifu na usimamizi mahili wa miradi ya maendeleo na kwamba wananchi wakipewa
hamasa na viongizi wao, watashiriki kikamilifu kutekeleza miradi yao
Aidha mkuu huyo wa mkoa ameanzisha kampeni maalumu ya
ufyatuaji na uchomaji wa matofali katika kila kijiji mkoani humo kwa lengo la
kuwa na benki ya matofari
Kanali Machibya amebainisha kuwa matofari licha ya kutumika
kujengea miundo mbinu ya huduma za jamii, pia ni chanzo cha mapato kwa vijana
mkoani Kigoma
Mkuu wa mkoa wa Kigoma alikuwa wilayani Kibondo kwa ziara ya
kikazi.