Baadhi ya dalili za ugonjwa wa Ebola ni kutokwa damu mwilini, mdomoni, puani,machoni nk |
Zaidi ya watu 399 wameripotiwa kupoteza maisha baada ya kuugua ugonjwa hatari wa Ebola katika nchi kadhaa za afrika magharibi.
Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO zilizokaririwa na mtandao wa PLEN MEDIA zaidi wa watu 635 wameambukizwa na kuugua ugonjwa huo unaoua haraka kuliko ugonjwa mwingine duniani.
WHO imetaja akuwa wengi kati ya waliofariki ni raia wa Liberia na Siera Lione na kwamba tahadhari zimechukuliwa zaidi ili kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo katika nchi jirani.
"Ni mlipuko wa hatari sana kuwahi kutokea katika ukanda huu" alisema Bw. Daniel Epstein, msemaji wa Shirika la Afya Duniani WHO.
Ameongeza kuwa hawezi kusema kuwa wameshindwa kudhibiti lakini udharula wa mlipuko huo umeamsha mamlaka za ulinzi wa afya ya jamii kuchukua hatua za dharuala kuokoa wagonjwa na kuzuia maambukizi zaidi.
Kiasi cha maafisa wa WHO 150 wako katika maeneo yaliyoathiriwa na Ebola wakishirikiana na wizara za afya katika nchi hizo, vituo vya afya na klinic za jamii pamoja na wadau wengine wa afya wa kimataifa kutoa matibabu na kinga.
WHO mwishoni mwa wiki imekutana na wadau wa afya kutoka nchi 11 za ukanda wa magharibi ambapo walikutana katika nchi ya Ghana na kujadili juu ya mlipuko huo na namna nchi za ukanda huo zinavyopaswa kulichukulia tukio hilo kwa namna ya pekee ili kunusuru vifo zaidi
Kwa habari zaidi bofya hapa ebola Africa