Kiongozi mmoja wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema,
amevamiwa na kushambuliwa na watu wasio julikana na kumjeruhi sehemu kadhaa za
mwili wake.
Taarifa za jeshi la polisi zimemtaja kiongozi huyo kuwa ni
Bw. Deogratius Luyunga mbaye ni makamu
mwenyekiti wa kamati ya uenezi kanda ya magharibi.
Imeelezwa kuwa watu wasiofahamika walimzingira usiku wa manane
wakati akitoka kuangalia mpira katika eneo la Mwanga mjini Kigoma.
Hadi sasa haijafahamika chanzo cha shambulizii hilo na
wahusika wake ingawa Bw. Luyunga anahusisha tukio hilo na masuala ya kisiasa.
Imeelezwa kuwa mhanga huyo wa shambulio alipigwa na kuchanwa sehemu mbalimbali za mwili wake kwa wembe kabla ya wasamaria wema kujitokeza na kumwokoa
Bw. Deogratius Luyunga anapata matibabu katika hospitali ya mkoa wa Kigoma Maweni na halii yake inaendelea vizuri