![]() |
Sehemu ya kijiji cha Mwasabuka wilayani Nyang'hwale mkoani Geita ilivyoharibiwa kutokana na uchimbaji wa Dhahabu, Nyumba zaidi ya 500 hatarini kutokana na kuathiriwa na milipuko ya fataki za kuvunja miamba ya madini hayo
Asasi ya Okoa Mazingira REMA iliyoko mkoani Geita imeitaka
serikali kufanya uchunguzi wa athari za mazingira zinazotokana na uchimbaji
mkubwa na mdogo wa madini ya dhahabu mkoani humo ili kunusuru maisha ya
wananchi
Rai hiyo imetolewa na katibu mtendaji wa asasi hiyo Bw. Idd
Malangula wakati akiongea na Uhuru FM kuhusu athari za mazingira katika eneo la
migodi ukanda wa ziwa Victoria
BW. Malangula
amebainisha kuwa asasi hiyo imebeini kuwepo kwa athari kubwa za kimazingira
zinazotokana na makampuni ya madini kutozingatia hifadhi kanuni, pamoja na
wachimbaji wadogo kutokuwa na elimu.
Amebainisha kuwa wananchi wanaopakana na migodi ya dhahabu
mkoani Geita wako katika hatari ya kupoteza maisha kwa kuugua maradhi
yanayotokana na matumizi ya maji yaliyochafuriwa na kemikali hatari kutoka
migodini
Aidha Bw. Malangula ametaja kuwa utafiti uliofanywa na asasi
yake katika bonde la mto Nyakabare wilayani Geita umebaini kuwepo kwa kemikali
za baruti, vumbi na viwatilifu hatari ambavyo huenda vikawadhuru binadamu.
Nyakabare ni mto pekee ambao unategemewa na wakazi wa vijiji
zaidi ya kumi na vine ambapo maji yake hutumika kwa matumizi ya nyumbani, kilimo
na mazingira na maji yake huelekea ziwa Victoria.
Bw. Malangula amebainisha kuwa licha ya makampuni ya madini
kutambua athari ya kimazingira na afya kwa binadamu, wameendelea kulipua baruti
na kutumia kemikari ambazo kuishia katika mto huo jambo ambalo ni hatari kwa
binadamu
Asasi ya REMA inayojishughulisha na hifadhi ya mazingira
mkoani Geita ni moja ya makundi ambayo yanapigwa vita na na vikundi vya
wachimbaji wadogo, wakubwa na taasisi za umma ambazo zinahusika na uharibifu
huo wa mazingira,