Bw. Philip Mangula (katikati) akiwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dr. Amani Kaborou (kushoto) na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Uvinza Bw. Muhamed Kabambe (kulia) |
Ziara ya makamu mwenyekiti wa ChamaCha Mapinduzi CCM Bw. Philip Mangula Imeingia dosari baada ya mmoja wa viongozi wa chama hicho wilayani Uvinza kufungwa jela baada ya kutumia vipaza sauti
Mahakama ya Mwanzo Nguruka wilayani Uvinza mkoani Kigoma,
imemhukumu kifungo cha mwezi mmoja Jela, katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama
Cha Mapinduzi wilaya ya Uvinza kwa kosa la kuipigia kelele mahakama.
Tukio hilo limetokea leo wakati kiongozi huyo Bw. Majaliwa
Zuberi alipotumia vipaza sauti ndani ya ukumbi wa CCM kutangaza ujio wa makamu
mwenyekiti wa CCM Taifa Bw. Philip Mangura katika wilaya hiyo
Kufuatia sauti hiyo kusambaa nje ya ukumbi huo, Hakimu William Kamugisha alitoa agizo la kukamatwa kwa Bw. Zuberi na kisha kumhukumu kwenda jela
kwa kosa la kuvuruga mahakama.
Hakimu Kamugisha anaeleza kuwa, Bw. Zuberi alikaidi agizo la mahakama lililomtaka apunguze sauti na kwamba alitoa majibu ya jeuri mbele ya mahakama hiyo.
Viongozi wa CCM mkoa wa Kigoma wamepinga vikali hukumu hiyo
na kueleza kuwa imegubikwa na hisia za kisiasa.
Wameeleza kuwa mwenezi huyo hakuwa eneo la mahakama hiyo, na
wamemtaka Bw. Mangula kuagiza mamlaka za dola kuchunguza uadilifu na utendaji
kazi wa hakimu huyo.