Taasisi ya
saidia wazee Tanzania SAWATA imewataka wazee kushirikiana na serikali za mitaa
kuunda mabaraza ya wazee katika ngazi za vijiji na mitaa.
Rai hiyo
imetolewa na katibu wa SAWATA wilaya ya Kasulu Bi. Cotrida Kokupima wakati
akitoa mada juu ya haki za wazee katika semina ya wazee watoa huduma za
wagonjwa majumbani.
Bi. Kokupima
amebainisha kuwa, kutokuwepo kwa mabaraza hayo kumechangia kukwama kwa juhudi
za wazee kudai haki zao hususani upatikanaji wa huduma za afya bure.
Bi. Cotrida Kokupima, Katibu Mtendaji SAWATA KASULU |
Aidha wazee
waliohudhuria semina hiyo wamekiri kukosa haki nyingi hususani za kiafya na
kiuchumi jambo ambalo ni hatari kwa uhai wao, na wameahidi kufuatilia uundwaji
wa mabaraza hayo.
Jumla ya
wazee 31 wawakilishi kutoka kata za Murufiti na Nyamidaho wilayani Kasulu
wamehudhuria semina hiyo ya utambuzi wa haki na wajibu.
Wakati huo huo Wito umetolewa kwa jamii kuwajali wazee kwa kuwapa huduma muhimu za kijamii ili kuwapunguzia msongo wa maisha
Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa asasi ya Saidia Wazee Tanzania wilayani Kasulu Mzee
Jackson Bukuru wakati akitoa mwongozo wa huduma kwa wazee wasiojiweza wilayani Kasulu
Mzee Bukuru amebainisha kuwa vijana wameacha desturi ya kuwahudumia wazazi wao jambo ambalo linachangia wazee kukata tamaa.
Amesisitiza kuwa, endapo vijana hawatarejesha moyo wa kujali wazee ni vema nao wasirejee kwa wazee wanapokuwa na matatizo au kuzidiwa kwa ugonjwa