Sehemu ya mji wa Kasulu barabara kuu iendayo Burundi kupitia Kijiji cha Heru juu |
Mwanamke mmoja mkazi wa kijii cha Herujuu wilayani Kasulu
mkoani Kigoma, amefariki dunia baada ya kushambuliwa na wananchi
Tukio hilo limetokea mapema leo baada ya kundi kubwa la
wananchi kuvamia makazi ya mwana mke huyo Bi. Apolonia Bwire na kuanza kumpiga
kwa mawe wakimtuhumu kuhusika na vitendo vya kishirikina
Jeshi la polisi wilaya Kasulu limethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kwamba limejaribu kumuokoa mama huyo akiwa amejeruhiwa vibaya na
kumkimbiza hospitali.
Muuguzi wa zamu katika hospitali ya wilaya ya Kasulu Bi.
Agnes Bukombe amethibitisha kufariki kwa mwanamke huyo na kutaja kuwa kifo
chake kimetokana na kuvuja damu nyingi.
Nyumba mbili za mwanamke huyo zimeteketezwa kwa kuchomwa moto
na mali mbalimbali kuporwa na namia ya wananchi waliozingira makazi hayo.