Na. Elsante John
Singida
MRADI wa michezo 'TTU-Education through sports', kupitia ufadhili
wa nchi ya Finland, unaendesha mafunzo ya siku tano ya mchezo wa riadha kwa
walimu wa shule za msingi na Sekondari Mkoani Singida.
Meneja mradi huo Anold Bugado amesema mafunzo hayo, chini ya chama
cha walimu nchini (CWT), ni mwendelezo wa taasisi hiyo kutoa elimu ya michezo kwa walimu hao,
lengo likiwa ni kuinua michezo mkoani Singida.
Bugado amesema kuwa mafunzo hayo ambayo yatawaimarisha walimu
katika kuwaandaa wanafunzi kumudu vyema mchezo huo na mingine ya aina mbalimbali, ameiomba
jamii na serikali kutunza vyema vifaa vinavyotolewa na taasisi yake.
Mafunzo hayo yanayofanyika Mjini Singida ambayo yalianza jumatatu yatafungwa kesho ijumaa, yanashirikisha
walimu 12 kutoka wilaya Mkalama, Iramba, Manispaa Singida, Manyoni, Ikungi na Singida
vijijini.
MWISHO.