HABARI MPYA
blink

399 WAMEPOTEZA MAISHA KWA UGONJWA WA EBOLA

Written By Unknown on Jumapili, 29 Juni 2014 | 13:21

Baadhi ya dalili za ugonjwa wa Ebola ni
kutokwa damu mwilini, mdomoni, puani,machoni nk

Zaidi ya watu 399 wameripotiwa kupoteza maisha baada ya kuugua ugonjwa hatari wa Ebola katika nchi kadhaa za afrika magharibi. 

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO zilizokaririwa na mtandao wa PLEN MEDIA zaidi wa watu 635 wameambukizwa na kuugua ugonjwa huo unaoua haraka kuliko ugonjwa mwingine duniani. 

WHO imetaja akuwa wengi kati ya waliofariki ni raia wa Liberia na Siera Lione na kwamba tahadhari zimechukuliwa zaidi ili kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo katika nchi jirani. 

"Ni mlipuko wa hatari sana kuwahi kutokea katika ukanda huu" alisema Bw. Daniel Epstein, msemaji wa Shirika la Afya Duniani WHO. 

Ameongeza kuwa hawezi kusema kuwa wameshindwa kudhibiti lakini udharula wa mlipuko huo umeamsha mamlaka za ulinzi wa afya ya jamii kuchukua hatua za dharuala kuokoa wagonjwa na kuzuia maambukizi zaidi.

Kiasi cha maafisa wa WHO 150 wako katika maeneo yaliyoathiriwa na Ebola wakishirikiana na wizara za afya katika nchi hizo, vituo vya afya na klinic za jamii pamoja na wadau wengine wa afya wa kimataifa kutoa matibabu na kinga.

WHO mwishoni mwa wiki imekutana na wadau wa afya kutoka nchi 11 za ukanda wa magharibi ambapo walikutana katika nchi ya Ghana na kujadili juu ya mlipuko huo na namna nchi za ukanda huo zinavyopaswa kulichukulia tukio hilo kwa namna ya pekee ili kunusuru vifo zaidi 

 Kwa habari zaidi bofya hapa ebola Africa

MASLAHI YA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA

Written By Unknown on Alhamisi, 26 Juni 2014 | 14:55

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria Kongamano la maadili lililoandaliwa na Baraza la habari Tanzania MCT mjini Bagamoyo.



Imeelezwa kuwa maslahi duni ya wafanyakazi wa vyombo vya habari kunatokana na kutokuwepo na chama cha wafanyakazi wa tasnia ya habari

Hayo yamebainishwa na katibu mtendaji wa Baraza la habari Tanzania Bw. Kajubi Mukajanga wakati akihitimisha kongamano la maadili ya uandishi wa habari mjini Bagamoyo leo.

Bw. Mukajanga amebainisha kuwa vyombo vingi vya habari haviwalipi ipasavyo watumishi wake na huchangia uandishi wa habari zisizozingatia weledi

Aidha amepongeza kuwepo mchakato wa kuanzisha chama cha wafanyakazi wa tasnia ya habari JUT na kuwahimiza waandishi wa habari kujiunga ili kuwa na nguvu.

KIGOMA KUANZISHA BENKI YA MATOFARI


Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kanali mstaafu Issa Machibya


Mkuu wa mkoa wa Kigoma kanali mstaafu Issa Machibya amewataka viongozi wa umma kuhakikisha wanasimamia ipasavyo utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ili kuwaondoa wananchi katika lindi la umasikini.

Agizo hilo amelitoa wilayani Kibondo mkoni humo jana katika ziara yake ya kukagua shughuli za maendeleo 

Kanali Machibya amebainisha kuwa, kipimo cha utumishi ni uadilifu na usimamizi mahili wa miradi ya maendeleo na kwamba wananchi wakipewa hamasa na viongizi wao, watashiriki kikamilifu kutekeleza miradi yao

Aidha mkuu huyo wa mkoa ameanzisha kampeni maalumu ya ufyatuaji na uchomaji wa matofali katika kila kijiji mkoani humo kwa lengo la kuwa na benki ya matofari

Kanali Machibya amebainisha kuwa matofari licha ya kutumika kujengea miundo mbinu ya huduma za jamii, pia ni chanzo cha mapato kwa vijana mkoani Kigoma

Mkuu wa mkoa wa Kigoma alikuwa wilayani Kibondo kwa ziara ya kikazi.

SIKILIZA MAKALA KUHUSU HOMA YA DENGUE TANZANIA

Written By Unknown on Jumapili, 8 Juni 2014 | 08:59


HII NDO DENGUE SIKILIZA


ANGALIA KAZI TULIZOFANYA WAKATI WA MAFUNZO KATIKA KITUO CHA RNTC- UHOLANZI


HIZI NI BAADHI YA KAZI AMBAZO TIMU YA WANAHABARI KUTOKA KARIBU PEMBEZOTE ZA DUNIA TULIOKUWA KATIKA MAFUNZO KATIKA CHUO CHA RNTC TULIFANIKIWA KUZIFANYA KATIKA MAZOEZI YETU






CERTIFICATE CEREMONY

SIKILZA SIMULIZI YA MAOINDUZI YA UKRISTO BARANI ULAYA-


Hii ni Makala maalumu yenye simulizi tamu inayohusu mtazamo na mabadiliko yimani ya kikristo Barani Ulaya. sikiliza na elimika.

UMOJA WA WAZAZI WAAZIMIA KUANZISHA SHULE KILA KATA

Written By Unknown on Alhamisi, 5 Juni 2014 | 05:47


Umoja wa wazazi wilaya ya Kasulu umeazimia kuanzisha shule za awali kila kata pamoja na vyama vya akiba na mikopo kwa dhamira ya kuinua kiwango cha ufahamu wa mabadiliko ya kimaisha pamoja na kipato cha kaya na kuepuka Rushwa nyakati za uchaguzi.

Imeelezwa kuwa uwepo wa vitendo vya rushwa katika chaguzi  mbalimbali kunatokana na jamii kutokuwa na elimu ya kutosha pamoja na umasikini ambao hutumiwa na wagombea kulaghai ili kupata kura

Umoja huo unaeleza kuamini kuwa endapo mfumo wa elimu za awali utaanzishwa katika ngazi cha chini pamoja na wazazi au kaya kuwa na kipato cha kutosha upo uwezekano wa wazazi kuwa na uwezo wa kupinga tabia za wanasiasa kuitumia fursa ya ujinga na umasikini kama chambo.

BODA BODA WAIIJIA JUU SERIKALI -WADAI ULINZI ZAIDI

Baadhi ya boda boda zikiwa nje ya ofisi ya CCm kasulu kulalamikia unyanyasaji





Umoja wa vijana wa CCM wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma umemtaka mkuu wa wilaya ya Kasulu kuitisha kikao cha kamati ya ulinzi na usalama kujadili mgogoro uliopo baina ya jeshi la polisi na vijana waendesha bodaboda.

Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa vijana wilaya Bw. Mberwa Chidebwe katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana mjini Kasulu kujadili mchakato wa katiba mpya

Bw. Mberwa ameeleza kuwa, waendesha pikipiki maarufu kama boda boda wamelalamikia kuwepo kwa uonevu na uvunjwaji wa sheria za usalama barabarani ambao hutekelezwa na baadhi ya askari wa jeshi la polisi

Ametaja uonevu huo kuwa ni kukamatwa hovyo na kuombwa Rushwa, kuzushiwa kesi za uongo, kuwekwa rumande kwa uda mrefu bila mashtaka na idara ya mahakama kuwahukumu kifungo kinyume cha sheria za usalama barabarani

Mkuu wa wilaya ya Kasulu Dani Makanga amekiri kupokea malalamiko hayo na kuahidi kuchukua hatua ili kutatua mgogoro huo

WANAHABARI TANZANIA WAKUMBUSHWA KUUNGANA - IFJ


Mr. Louis Thomas - officer from International Federation for Journalists - IFJ addressing the Tanzania journalists during the seminar on crating a journalists union in Tanzania


Dar es salaam
By. Prosper Kwigize

Waandishi wa habari nchini Tanzania wamehimizwa kuungana na kutambua haki zao ili kujiendeleza kitaaluma na kimaslahi.

Rai hiyo imetolewa na afisa kutoka jumuiya ya kimataifa ya waandishi wa habari IFJ Bw. Louis Thomas wakati akitoa ujumbe wa umuhimu wa vyama vya wafanyakazi wa tasnia ya habari katika kikao cha wanahabari nchini jijini Dar es salaam leo.

Bw. Thomas amebainisha kuwa, malipo madogo yasiyolinganga na thamani ya taaluma katika nchini nyingi za afrika kunatokana na wanahabari wenyewe kutotambua wajibu na haki zao katika jamii.

Amesisitiza kuwa kuundwa kwa chama cha wafanyakazi wa sekta ya habari kutawasaidia waandishi na watumishi wa vyombo vya habari kudai na kupata haki za msingi kulingana na weledi wao.

Hata hivyo IFJ imeonya kuwepo kwa baadhi ya waandishi wa habari wasio na ujuzi ambao huharibu wasifu wa taaluma hiyo.
 
Shukrani kwa : Harold Dickson | Prosper Kwigize | 0752490120
Copyright © 2013. KWIGIZE NEWS AND COMMUNICATION - Haki zote zimeifadhiwa
Email us: kwigizenews@gmail.com
0764243377