Muziki ni moja kati ya sanaa muhimu sana ambazo zimekuwa
kivutio katika burudani miongoni mwa jamii ndani na nje ya Tanzania.
Muziki umekuwa pia ukitumika katika kuibua mjadala, kuchochea
maendeleo pamoja na kueneza habari Fulani kwa jamii.
Wanasiasa pia wamekuwa wakiwatumia wasanii katika kueneza
sifa zao na propaganda za vyama vyao ili kushawishi wananchi kuzikubali sera
zao na kuwachangua katika nafasi wanazoomba.
Nchini Tanzania muziki umekuwa ukibadilika siku hadi siku
ukihama kutoka katika ushairi wa kawaida wa kuelimisha jamii na kuhamia katika
mapenzi zaidi, baadhi ya wasanii huimba mapenzi tu na wengine huchanganya
mapenzi na masuala mengine ya kijamii.
Wasanii wengine huimba tu ilimradi waamshe hisia za kucheza
hata kama wimu unaoimbwa hauna maudhui yoyote zaidi ya kukolezwa na vyombo vya
kisasa vya kutengeneza milindimo na vionjo vitamu.
Katika makala haya nimevinjali baadhi ya nyimbo za Diamond
kutoka Tanzania na kupata hoja ya kukueleza.
Wasanii kote Tanzania wameaminishwa na wapenzi wao
(wasikilizaji na watazamaji wa muziki) na sasa wanadhani nyimbo nzuri ni ile
inayoimba mapenzi na kutonesha ama kidonda cha penzi au kuanzisha hisia mpya ya
mapenzi.
Ni kwa sababu hiyo wengi wao wamekuwa wakitunga na wakiimba nyimbo za mapenzi tu, na
kwa bahati mbaya wanasahau mambo mengine ya kijamii.
Diamond katika wimbo wake wa Mbagala, alifanya muziki wenye
muonekano na vionjo vya mapenzi lakini ndani yake kuna jambo muhimu sana la
kijamii, ambalo nina hakika ndilo linabeba maudhui yote ya wimbo wake.
Diamond anamkosa mrembo aliye mpenda sana kwa sababu
mazingira anapoishi ni machafu na hatari kwa afya za wakazi wa maeneo ya
Mbagala
Angalia video hii na utume maoni yako bofya hapo kwenye neno mbagala uone kisha tutumie maoni yako kuhusu wimbo huo na maudhui yake, anuani yetu ni plen.media@gmail.com