Sanamu ya Ndege iliyoungwa na mmoja wa wanasayansi chipukizi wa Tanzania |
Na. Mwandishi wetu
Dar es Salaam
Maonesho pamoja na sherehe ya kuwatunukia zawadi
washindi wa wanasayansi chipukizi au Young Scientists Tanzania (YST)
yalifanyika tarehe 13 hadi 14 mwezi Agosti
katika ukumbi wa Aghakhan Diamond Jublee.
Maonesho haya walifadhiliwa na British Gas Tanzania pamoja na Irish Aid kwa matarajio kuwa vijana hawa wakiendelezwa tatizo la afrika kukosa wana sanyansi litakwisha
Mgeni rasmi wa maonesho hayo alikua Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dr. Mohammed Gharib Bilal akifuatana na Balozi
wa Ireland nchini Tanzania Finneoula Gilsenan pamoja na Waziri Prof. Makame M.
Mbarawa ambao pia walihudhuria maonesho hayo
Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal akisalimiana na meneja wa kampuni ya British Gas Bw. Adam Prince wakati wa Maonyesho hayo |
Wanafunzi 200
na walimu kutoka mikoa mbalimbali Tanzania walikusanyika jijini Dar es Salaam
kuonyesha miradi yao ya utafiti mwaka huu.
Ongezeko la msaada unaotolewa na BG(British Gas) Tanzania na Ireland Aid (Shirika
la msaada la Ireland),kumewezesha maonyesho ya wanasayansi chipukizi kuwafikia wanafunzi vijana kwa wingi zaidi ndani ya mwaka huu 2014.
Maonyesho ya( YST ) 2014 ni muendelezo wa mafanikio
yaliyofikiwa miaka ya nyuma kutoka shule 4 mwaka 2011 hadi kufikia shule 100 mwaka huu.
Robn Damas na Michael Laurent wanafunzi kutoka Ilboru sekondari wakifurahia tuzo |
Programu ya YST ilitokana na
jitihada za Ireland ambayo ilitumia mfumo wa maendeleo ya elimu kupitia (CDPC)
Combat Diseases of Poverty Consortium. (Kundi
la kupambana na maradhi yanayotokana na umaskini.
Wanafunzi watakaoshinda watawezesha shule zao kukua
kisayansi na maendeleo. Zawadi zilizomo ni laptops, fedha, scholarships, pamoja
na vitabu kwa maktaba za shule. Washindi wa jumla wa YST 2014 wataalikwa kuhudhuria maonyesho
ya BT Young Scientists na Teknolojia yatakayofanyika nchini Ireland mnamo Januari 2015.
Kila mwaka maonyesho YST yanalenga kuongeza mafanikio katika jitihada za kuinua kiwango cha elimu ya sayansi katika
shule za sekondari Tanzania .
Maonyesho
yanaelezea miradi kutoka makundi mbalimbali ya sayansi,
kibaiolojia na ikolojia; fizikia na kemia; masomo ya kijamii na kitabia; na
teknolojia.
Young Scientists Tanzania inatoa wito kwa shule zote
nchini kujipatia fursa ya kukua kisayansi na kubadilisha mfumo wa kujifunza masomo
ya Sayansi kwa kupitia mashindano hayo. Mashinda hayo hufanyika kila mwaka
jijini Dar es Salaam na huhusisha zaidi ya shule 100.