HABARI MPYA
blink
18:09
KENYA YAZINDUA UJENZI WA RELI KUELEKEA UGANDA NA RWANDA
Written By Unknown on Jumamosi, 30 Novemba 2013 | 18:09
Kenya imezindua rasmi ujenzi wa njia ya Reli itakayounganisha kanda ya Afrika Mashariki na eneo la maziwa makuu ujenzi utakaofadhiliwa na serikali ya China.
Reli hiyo itaunganisha Kenya na Sudan Kusini, DR Congo na Burundi.
Sehemu ya kwanza ya njia hiyo ya reli , itaunganisha bandari ya Mombasa na Mji mkuu Nairobi na kupunguza muda wa safari kati ya miji hiyo kutoka masaa 15 hadi masaa manne tu.
Huu bila shaka ndio utakuwa mradi mkubwa Zaidi kuwahi kujengwa tangu nchi hiyo kujipatia uhuru miaka 50 iliyopita.
Mradi huo utagharimu dola bilioni 5.2 kiasi kikubwa cha pesa hizo kikitolewa na Uchina.
Baadhi ya wakenya wanalalamika kuwa tenda hiyo imetolewa kwa kampuni ya kichina kwa njia isiyofaa.
Rais Uhuru Kenyatta katika hafla ya uzinduzi huo amesema kuwa mradi huu ndio utakuwa kumbukumbu kubwa ya utawala wake Kenya.
Mkataba wa ujenzi wa njia hiyo ya reli, ulifikiwa kati ya Rais Kenyatta na mwenzake wa China Xi Jinping mnamo mwezi Agosti mjini Beijing.
Pia kuna matumaini kuwa njia hiyo ya reli itapunguza msongamano mjini Mombasa moja ya bandari yenye shughuli chungu nzima barani Afrika.
Njia ya reli iliyoko sasa, ni ile iliyojengwa enzi za ukoloni.
Baada ya kukamilika kwa sehemu ya kwanza ya reli hiyo mjini Nairobi, mwaka 2017, itaendelezwa hadi Magharibi mwa DRC hususan mjini Kisangani, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.
"Tunachokifanya hapa leo, kitaleta mageuzi makubwa sio nchini Kenya tu bali katika kanda nzima ya Afrika Mashariki,’’ alisema Rais Kenyatta akitaja mradi huo kama jambo la kihistoria.
Aliongeza kusema kuwa mradi huu ni moja ya miradi mikubwa katika maono yake ya maendeleo itimiapo mwaka 2030 kuboresha hali ya miundo msingi nchini humo.
Labels:
Development stories
07:57
GAZETI LA MWANANCHI 30, NOV
HABARI KUU
Mishahara ya vigogo ‘hailingani na ufanisi’
Posted 15 hours ago
Ripoti mpya ya utafiti imebainisha kuwa mishahara mikubwa wanayolipwa viongozi wa juu serikalini na wanasiasa hailingani na utendaji wao wa kazi....
Toa Maoni
KITAIFA
Uwekezaji: Gesi, madini juu, kilimo chaanguka
Posted 14 hours ago
Taarifa ya Uwekezaji Tanzania mwaka 2012 imetaja kuporomoka kwa kilimo huku madini na nishati zikiongezeka kwa kiasi kikubwa....
KITAIFA
Ushahidi wa umiliki Ziwa Nyasa watolewa
Posted 14 hours ago
Wasuluhishi wanazitaka Malawi na Tanzania kutoa majibu ya maswali manne muhimu wakati wakiwasilisha ushahidi wao kuhusu umiliki...
KITAIFA
Sarafu moja EAC kujadiliwa leo
Posted 14 hours ago
Wakuu wa Nchi Tano Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), leo Novemba 30, wanatarajiwa kutia saini mkataba wa kuwa na...
- Uchaguzi mkuu wa BFT leo
- Mzungu wa Simba kutua kesho
- Poulsen: Uwanja ulituangusha
- Eritrea yatumia ‘Mapro’
- Nyasi za uwanja zazidiwa
- Zanzibar Kanyaga twende
- Nyota watano kuondoka Yanga
- Mfumo sahihi wa kuendeleza vipaji unahitajika
- Elimu kikwazo kwa wajasiriamali nchini
- Mashirika yalia uharibifu wa mazingira
Labels:
Events
07:44
AFRIKA MASHARIKI NAYO KAMA ULAYA-SARAFU MOJA KUANZISHWA
Baada ya sintofahamu ya muda mrefu kuhusu jumuiya ya afrika
mashariki kuwa na sarafu moja, hatimae wakubwa leo wanasaini mkataba wa sarafu
moja ya afrika mashariki
Hatua hii inakuja huku kukiwa na vuguvugu la baadhi ya nchi
kutaka kuzitenga nyingine katika harakati za ukuaji wa uchumi wa afrika
mashariki pamoja mahusiano ya kisiasa miongoni mwao
Katibu mkuu wa jumuiya hiyo yenye makao makuu yake mkoani Arusha
nchini Tanzania Bw. Richard Sezibera amekaririwa na vyombo vya habari mapema
leo akieleza kuwa wakuu wan chi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi wanasaini
mkataba huo katika viwanja vya kilolo au Uhuru mjii Arusha
Labels:
siasa
07:24
PANGUA PANGUA JESHI LA POLISI TANZANIA
IGP Said Mwema (Mkuu wa jeahi la Polisi Tanzania) |
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema amefanya
mabadiliko ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera pamoja na baadhi ya Wakuu wa
Upelelezi wa mikoa na wakuu wa Polisi wa Wilaya katika baadhi ya mikoa
hapa Nchini.
Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Philipo Kalangi amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam, kuwa Mkuu wa kikosi cha kusimamia usalama wa Mazingira na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) George Mayunga ambaye alikuwa Mkuu wa kikosi cha kusimamia mazingira Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.
Aidha, baadhi ya Wakuu wa Upelelezi wa mikoa (RCO) na wakuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) waliobadilishwa ni pamoja na
Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Philipo Kalangi amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam, kuwa Mkuu wa kikosi cha kusimamia usalama wa Mazingira na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) George Mayunga ambaye alikuwa Mkuu wa kikosi cha kusimamia mazingira Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.
Aidha, baadhi ya Wakuu wa Upelelezi wa mikoa (RCO) na wakuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) waliobadilishwa ni pamoja na
aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa
Tabora ACP Edward Bukombe amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam,
Mkuu wa Upelelezi wa mkoa wa Geita (RCO) ACP Francis Kibona amehamishiwa
mkoa wa Njombe kuwa mkuu wa Upelelezi mkoa na nafasi yake inachukuliwa na
SSP Simon Pasua kutoka Makao makuu ya Upelelezi Dar es Salaam.
Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) ya Wanging’ombe SSP. Francis Maro amehamishiwa Mkoa wa Katavi kuwa Mkuu wa upelelezi wa mkoa na aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Katavi ACP. Emmanuel Nley amehamishiwa kikosi cha Polisi wanamaji Dar es Salaam. Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Rukwa SSP. Peter Ngussa amehamishiwa Makao makuu ya Upelelezi Dar es Salaam, nafasi yake inachukuliwa na SSP Alan Bukumbi aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Njombe.
Aliyekuwa Mkuu wa Polisi wilaya ya kati( OCD) Mrakibu wa Polisi (SP) Salum Ndalama anaenda kuwa kaimu mkuu wa upelelezi mkoa wa Tabora na aliyekuwa mkuu wa Polisi wa wilaya ya Tunduru (OCD) SP. Amadeus Tesha anakwenda kuwa Mkuu wa upelelezi kikosi cha Polisi reli.
Uhamisho huo ni wa kawaida katika kuboresha utendaji kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) ya Wanging’ombe SSP. Francis Maro amehamishiwa Mkoa wa Katavi kuwa Mkuu wa upelelezi wa mkoa na aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Katavi ACP. Emmanuel Nley amehamishiwa kikosi cha Polisi wanamaji Dar es Salaam. Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Rukwa SSP. Peter Ngussa amehamishiwa Makao makuu ya Upelelezi Dar es Salaam, nafasi yake inachukuliwa na SSP Alan Bukumbi aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Njombe.
Aliyekuwa Mkuu wa Polisi wilaya ya kati( OCD) Mrakibu wa Polisi (SP) Salum Ndalama anaenda kuwa kaimu mkuu wa upelelezi mkoa wa Tabora na aliyekuwa mkuu wa Polisi wa wilaya ya Tunduru (OCD) SP. Amadeus Tesha anakwenda kuwa Mkuu wa upelelezi kikosi cha Polisi reli.
Uhamisho huo ni wa kawaida katika kuboresha utendaji kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Labels:
News
01:19
World AIDS Day 2013 Statement by Donald Kaberuka, President of the African Development Bank Group
PRESS RELEASE
World AIDS Day 2013 Statement by Donald Kaberuka, President of the African Development Bank Group
World AIDS Day is December 1
TUNIS, Tunisia, November 29, 2013/ -- Africa has made significant progress in fighting the HIV/AIDS pandemic. In the past seven years, AIDS-related deaths declined by 32%.The number of people contracting the HIV infection declined by 25% in the past 10 years. The rate of mother-to-child transmission of HIV has also declined from 35% in 2001 to 26% in 2010. Ten years ago, we had fewer than 50,000 people on ARV treatment; today we have over 6 million receiving treatment. A few years ago, Senegal and Uganda were the only success stories for their outstanding results and containment of HIV; now we have 25 countries that lowered HIV infections by more than 50%. A lot has been achieved; however, the risks are far from over. Indeed, new infections are a threat. It is time to raise, not to lower our vigilance.
Photo Donald Kaberuka: http://www.photos.apo-opa.com/plog-content/images/apo/photos/donald-kaberuka-afdb-president.jpg
Recall, 30 years ago, when the first HIV-positive case was reported; 24 million Africans have lost their lives. Africa still bears the heaviest burden of the disease globally and accounts for 91% of the world’s children with HIV, 89% of HIV orphans and 69% of people living with HIV. Each day, 3,500 Africans die of AIDS and millions of others and their families and communities go through economic, psychological and social traumas. HIV-related stigma still hurts people, in society, in their workplaces and homes. Women in Africa are more severely affected than men. In 2012, 58% of people living with HIV were women.
HIV/AIDS continues to have a huge detrimental impact on the most important resource of our continent: our people. It robs the continent of vitally needed skilled workers and deprives families of their incomes. It has hampered our ability to educate and build our human capital. Kenya lost an estimated 1.7% of its teachers between 2000 and 2010 due to HIV/AIDS.
For the African Development Bank, in partnership with governments, international organizations, civil society and the private sector, the future of HIV/AIDS agenda is about ‘getting to zero’. Zero new HIV infections, zero discrimination and zero AIDS-related deaths. Getting there is not easy and the Bank aims to support African countries to, first, take ownership of the AIDS response. It is time for Africa to take bold steps to reduce dependence on external donors and work towards more sustainable domestic solutions. According to UNAIDS, Africa will require between US $11 billion and $12 billion for its AIDS response by 2015. Yet international funding to HIV is dwindling, putting our progress at risk.
Second, the Bank supports African countries in increasingly applying ‘value for money’ and ‘solidarity’ principles to strengthen social systems. The way HIV resources are mobilized and spent needs to change. The vertical approach may no longer be appropriate and cost-effective in many contexts. There is a need to mainstream AIDS-related services into the general healthcare delivery systems and to support the local production of ARVs.
Third, the Bank supports the building of inclusive health systems to fight stigma and discrimination. Let us all tackle stigma and discrimination by building a supportive and caring culture both in their communities and workplaces. We cannot leave the victims of HIV/AIDS and their families behind.
Finally, the Bank, through its inclusive growth agenda, aims to support the reduction of women’s increased vulnerability and prevent mother-to-child HIV transmission. Addressing the gender dimension is an important priority in the response to the epidemic. Recent progress suggests that the solutions are in our hands. We can reduce gender inequalities by empowering women with information and services to prevent and treat HIV. Strategies to counter and manage gender-based violence can be effectively included in HIV-prevention programs. Effective treatment to reduce mother-to-child HIV transmission now needs to be scaled up and made accessible to those who need them, regardless of their socioeconomic status. Training health workers to provide gender-friendly counseling and services must also be prioritized. Most importantly, we need to sensitize men and elicit their involvement to create a supportive environment for reducing women’s vulnerabilities to the epidemic.
Getting to zero starts with us. It is time for Bank staff to take care of themselves and their families by taking advantage of HIV/AIDS services the Bank’s Medical Centre provides. These include Anonymous Voluntary Confidential Counseling and testing available to all Bank staff and their families.
I also want to stress that the African Development Bank is a workplace of zero discrimination and that we must support each other in our communities and workplace. Our fight to get to zero is producing results. Let’s continue in order to give the next generation of Africans – our children, our sons and daughters -- an AIDS-free life ahead. Zero has a value!
Donald Kaberuka, President of the African Development Bank Group
Distributed by APO (African Press Organization) on behalf of the African Development Bank (AfDB).
SOURCE
African Development Bank (AfDB)
Labels:
News
13:30
Tuhuma zang’oa maofisa Maliasili
Written By Unknown on Ijumaa, 29 Novemba 2013 | 13:30
Na Elizabeth Edward, Mwananchi
Posted Alhamisi,Novemba28 2013 saa 10:23 AM
Posted Alhamisi,Novemba28 2013 saa 10:23 AM
Kwa ufupi
- Akizungumza baada ya kufungua warsha ya wadau wa wanyamapori jana, Balozi Kagasheki alisema mapambano dhidi ya ujangili yanakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na kuhusisha mtandao mkubwa ambao ndani yake kuna watu wazito na vigogo serikalini.
Dar es Salaam. Waziri wa
Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki amesema wizara yake
imewasimamisha kazi baadhi ya maofisa kutokana na kujihusisha na
biashara haramu ya ujangili wa meno ya tembo.
Akizungumza baada ya kufungua warsha ya wadau wa
wanyamapori jana, Balozi Kagasheki alisema mapambano dhidi ya ujangili
yanakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na kuhusisha mtandao mkubwa
ambao ndani yake kuna watu wazito na vigogo serikalini.
“Biashara hii wacha bwana, ni ngumu kwelikweli,
inahusisha mtandao mkubwa… tayari tumewasimamisha baadhi ya watumishi na
hivi karibuni nitayaweka wazi majina ya vigogo na watu wengine
wanaojihusisha na mtandao huu.
“Haitaishia kuwasimamisha kazi tu, hatua zaidi
dhidi yao zitachukuliwa kwani kujihusisha na vitendo vya ujangili ni
sawa na kuhujumu uchumi wa Watanzania,” alisema Balozi Kagasheki.
Hata hivyo, Balozi Kagasheki amekuwa akitoa ahadi ya kuwataja vigogo wanaojihusisha na ujangili bila kutekeleza.
Kauli hiyo ya Kagasheki imekuja zikiwa zimepita
wiki tatu tangu Rais Jakaya Kikwete kusitisha kwa muda Operesheni
Tokomeza, lengo likiwa ni kutoa nafasi kwa Serikali kujipanga na
kurekebisha kasoro zilizojitokeza kwenye awamu ya kwanza ya operesheni
hiyo.
Balozi Kagasheki alisema rushwa na kukosekana kwa
utashi wa kisiasa ndiyo sababu inayochangia kuwapo kwa changamoto kubwa
katika vita dhidi ya biashara hiyo haramu, inayohatarisha maisha ya
tembo na soko la utalii.
“Hii ni rasilimali ya Watanzania, hivyo hatutaweza kuvumilia watu wachache wanufaike,” alisema.
- ARV: Mapinduzi ya kitiba yanayosaidia maelfu nchini
- Lucy: Nina amani ingawa nina VVU
- Vidonge vya Uzazi wa Mpango vyadaiwa kusababisha upofu
- Watanzania changamkieni fursa hizi Burundi
- Wakala adai Simba ilimbania Juma Kaseja
- Kili Stars, Zambia ngoma droo
- Yanga, Simba, Azam kuchuja ‘mapro’ wao
- Wawekezaji katika gesi, mafuta wakidhi vigezo
- Tanga wamtetea Zitto, Iringa waitetea Chadema
- Wasiotahiriwa chanzo cha Ukimwi nchini
- Baregu aitahadharisha Chadema kuhusu Zitto
- Kenyatta apoza hasira za Kikwete
- Kapteni Mstaafu Robert: Sitasahau nilipohukumiwa maisha jela
- Waraka wa Chadema utata mtupu
- Serikali yatangaza nafasi za kazi 1,100
- Alikuja Dar kama ‘house boy’ sasa ametajirika
- Nafasi za kazi
- Tanzania, DRC, Burundi kushirikiana
- Watanzania changamkieni fursa hizi Burundi
- ‘Afrika Kusini sasa tishio kwa vijana’
- Lucy: Nina amani ingawa nina VVU
Labels:
siasa