Imeelezwa kuwa mfumo dume ni moja ya changamoto
zinazokwamisha wananwake nchini Tanzania katika harakati za kushiriki uongozi
wa kijamii na uchumi.
Hayo yamebainishwa na afisa kutoka shirika la umoja wa
mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, Bi. Rose Mwalimu katika
mahojiano maalumu.
Bi. Rose amebainisha kuwa wanawake wananyimwa fursa kutokana
na mfumo dume jambo ambalo linatia shaka kama usawa wa hamsini kwa hamsini
utapatikana ifikapo 2015 katika uwakilishi wa vyombo vya maamuzi.
Aidha Bi. Rose amebainisha kuwa licha ya jamii kutegemea
vyombo vya habari katika kubadili tabia kwa njia ya habari, bado waandishi wa
habari Tanzania havijatoa mchango wake kuondoa mfumo dume na unyanyasaji wa
kijinsia
Akielezea juu ya weledi wa waandishi wa habari Tanzania Bi
Rose mwalimu ambaye pia kitaaluma ni veteran katika taaluma ya habari,
amewatahadharisha waandishi wa habari kuwa makini na waepuke kuandika habari
zenye kuchochea migogoro.
Shirika la UNESCO linaendesha mafunzo kwa waandishi wa
habari kutoka katika Radio jamii nchini ili kuwajengea uwezo wa kuandika habari
na kuandaa vipindi kwa kuzingatia masuala ya jinsi na jinsia.
Zaidi ya Radio Jamii 11 zimepata udhamini wa mafunzo na
kujengewa uwezo na UNESCO ambayo yamefanyika kati ya September 22 na October
mosi ambayo yamefanyika mkoani Kigoma pamoja na Mwanza.