Katika hali isiyotarajiwa na wengi, msanii maarufu Elizabeth maarufu LULU leo amekiri katika mahakama kuwa alimuua bila kukusudia msanii marufu Tanzania Steven Kanumba

Lulu ameieleza mahakama kuwa, Kanumba licha ya kuwa bosi wake alikuwa pia mpenzi wake na kwamba ulipotokea ugomvi na lulu kumpiga na kitu kizito Kanumba, alitoa taarifa kwa shemeji yake (mdogo wa Kanumba) kabla ya kukamatwa na polisi
wakili upande wa serikali Monica Mbogo amesema mashahidi kadhaa wapo tayari kutoa ushahidi juu ya Lulu kumua Kanumba kwa makusudi
Lulu alifikishwa kwa mara ya kwanza mahamani April 11 mwaka 2012 ambapo alisomewa shitaka la mauaji na kulazimika kukaa rumande kwa miezi sita kabla ya kupata dhamana