HABARI MPYA
blink

SECRETARY-GENERAL’S STATEMENT ON THE DEATH OF NELSON MANDELA

Written By Unknown on Jumamosi, 7 Desemba 2013 | 11:50

UN Secretary General Ban Ki Moon


Nelson Mandela was a singular figure on the global stage -- a man of quiet dignity and towering achievement, a giant for justice and a down-to-earth human inspiration.  

I am profoundly saddened by his passing.  On behalf of the United Nations, I extend my deepest condolences to the people of South Africa and especially to Nelson Mandela’s family and loved ones.

Many around the world were greatly influenced by his selfless struggle for human dignity, equality and freedom.  He touched our lives in deeply personal ways.  At the same time, no one did more in our time to advance the values and aspirations of the United Nations.  

Nelson Mandela devoted his life to the service of his people and humanity, and he did so at great personal sacrifice.  His principled stance and the moral force that underpinned it were decisive in dismantling the system of apartheid.
 
Remarkably, he emerged from 27 years of detention without rancor, determined to build a new South Africa based on dialogue and understanding. The Truth and Reconciliation Commission established under his leadership remains a model for achieving justice in societies confronting a legacy of human rights abuses.

In the decades-long fight against apartheid, the United Nations stood side-by-side with Nelson Mandela and all those in South Africa who faced unrelenting racism and discrimination. His 1994 address to the General Assembly as the first democratically elected President of a free South Africa was a defining moment. The Assembly has declared 18 July, his birthday, “Nelson Mandela International Day”, an annual observance on which we recognize and seek to build on his contributions to promoting a culture of peace and freedom around the world.

I was privileged to meet Nelson Mandela in 2009.  When I thanked him for his life’s work, he insisted the credit belonged to others.  I was very moved by his selflessness and deep sense of shared purpose.

Nelson Mandela showed what is possible for our world and within each one of us -- if we believe, dream and work together.  

Let us continue each day to be inspired by his lifelong example and his call to never cease working for a better and more just world.

New York, 5 December 2013

MAANDAMANO MAKUBWA KIGOMA KUPINGA ZIARA YA DR. SLAA MKOANI HUMO

Polisi wakipiga doria kulinda waandamanaji ilikusitokee vurugu au uvunjaji wa amani katika manspaa ya Kigoma ujiji (picha kwa hisani ya Hamis full migebuka -Kigoma)

Mamia ya wakazi wa mji wa Kigoma na vitongoji vyake leo wameandamana katika mitaa mbalimbali pamoja na kuchoma bendera na kadi za chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kupina ziara ya katibu mkuu wa chama hicho Dr. wilborad Slaa

Hatua hiyo ya maandamano ni ya pili kufanyika mjini Kigoma hususani katika jimbo la Kigoma Kaskazini kwa kile kinachotajwa kuwa ni kupinga kuvuliwa uongozi mbunge wa Kigoma kaskazini Zitto Kabwe

Imeelezwa kuwa maandamano hayo yanasisitiza kutokukubaliana na uamuzi wa kamati kuu ya CHADEMA kumuondoa Zito katika nafasi ya Naibu katibu mkuu na naibu kiongozi wa upinzani Bungeni

Katibu mkuu wa CHADEMA Dr. wilbroad Slaa yuko Mkoani Kigoma tangu juzi na amekuwa akikumbwa na dhahama la mabango na kuzomea katika maeneo aliyokwenda kuhutubia

Aidha katika hali ya kushangaza, leo amehutubia katika maeneo ya vijijini na kuruka maeneo yenye watu wengi katika wilaya ya Kasulu ingawa imeelezwa kuwa jumapili ndipo atahutubia mjini Kasulu


Vuguvugu la kupinga ziara hiyo bado linadhihirisha miongoni mwa wafuasi cha chama hicho ikiwa ni pamoja na Baraza la Vijana la Chadema BAVICHA ambao inaelezwa kuwa wamejiandaa kufanya vurugu, kuzomea na kumunyoshea mabango Dr. Slaa 

KIGOMA WADHAMIRIA KUMWANDIKIA BARUA RAIS KIKWETE

Barabara mpya ya Lami inayounganisha Tanzania na nchi ya Burundi kutokea mjii Kigoma

Mkoa wa Kigoma umeazimia kumwandikia Barua ya pongezi na shukurani Rais Jakaya Kikwete kwa kuwezesha mkoa huo kupata barabara za lami zinazotarajiwa kuunganisha mkoa huo na mikoa mingine ya Tanzania pamoja na nchi za jirani

Azimio hilo limefikiwa wiki hii mjini Kigoma wakati wa kikao cha Bodi ya Barabara baada ya wajumbe wa Bodi hiyo kubaini kuwa serikali ya awamu ya nne imedhamiria kuufingua mkoa huo kwa njia ya kujenga na kuimarisha miundombinu hususani barabara

Akitoa tamko hilo la dhamira ya kumshukuru Rais Mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni mwenyekiti wa Bodi ya barabara mkoani humo kanali Mstaafu Issa Machibya amebainisha kuwa serikali imeonesha dhamira ya kuimarisha miundombinu ili kupanua uchumi wa mkoa na taifa



Kwa upande wake meneja wa Tanroads mkoa wa Kigoma mhandisi Narcis Choma amebainisha kuwa kwa sasa mkoa wa Kigoma una kiasi cha kilomita 1,205.38 za barabara zote katika mkoa mzima

Mhandisi Choma amefafanua kuwa katika urefu wa barabara hizo ni kilomita 182.54 pekee ndizo zimejengwa kwa kiwango cha lami wakati kilimita 1,040.44 ni za changarawe na udongo.

Aidha katika kikao hicho, wenyeviti wa halmashauri za wilaya za Kakonko na Kasulu Bw. Juma Maganga na William Luturi wamempongeza meneja wa TANROADS Kigoma kwa utendaji mzuri wa kazi za ufuatiliaji na usimamizi wa ujenzi wa Barabara

Hata hivyo wenyeviti hao wameiomba serikali kuwekeza katika ujenzi wa barabara kuu ya kutoka Kidahwe hadi Nyakanazi na kusisitiza kuwa pamoja na kurahisisha mawasiliano, barabara hiyo ndiyo inayohusika na uchumi wa wanakigoma tofauti na ile inayojengwa kutoka Kigoma kwenda Tabora ambako sehemu kubwa ya eneo hilo ni msiti wa hifadhi


Wamesisitiza kuwa barabara ya Kigoma, Kasulu, Kibondo, Kakonko hadi Nyakanazi ndiyo barabara muhimu kwa uchumi wa mkoa wa Kigoma kutoka na kile kinachotajwa kuwa inapita katika makazi ya watu na eneo la soko la mazao ya mashambani.

NELSON MANDELA AAGA DUNIA

Written By Unknown on Ijumaa, 6 Desemba 2013 | 04:22



Kuanzia alfajiri ya leo December 06 2013, bendera ya taifa Tanzania pamoja nay a chama cha mapinduzi kinachotawala serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania zinapepea nusu mlingoti kuashiria kuwepo kwa tukio la simanzi au msiba kwa taifa hilo.

Upepeaji huo wa bendera nusu mlingoti ni matokeo ya utekelezaji wa agizo la Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete alilotoa usiku wa kuamkia leo muda mfupi baada ya rais wa Africa kusini Jacob ZUma kutangazia ulimwengu kuwa baba wa Taifa la Africa kusini na afrika Nelson Madiba Mandela amefariki dunia

Pembe zote za Tanzania zimeshikwa na simanzi kubwa kufuatia kifo cha Baba wa Taifa rafiki kwa Tanzania, watanzania wamekuwa na maoni tofauti kuhusu kifo hicho huku wengine wakidiriki kutaja kuwa nuru ya afrika sasa imegeuka giza nene kutokana na kifo cha Nelson Mandela

Kutoka hapa Tanzania eneo la mkoa wa Kigoma nimekutana na baadhi ya waombolezaji ambao hwasiti kutoa hisia zao

“Mandela ni mtu muhimu kwa bara la afrika, amekuwa kiongozi mwadilifu na mwaminifu kwa nchi yake na kwa afrika nzima” Lucas Yona mkazi wa Kasulu

Huyo ni mmoja wa wanaume ambao wanakiri kuwa baba wa taifa lla afrika ambalo hadi anaondoka angependa kuwepo na umoja wenye nguvu ya kisiasa na kiuchumi

Wanawake nao hawako nyuma katika kuenzi mchango wa Mandela katika ustawi wa afrika, huyu hapa ni mwanamke mwanaharakati na kiongozi wa umoja wa wanawake katika eneo la wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma

Grace Mbwiriza ni katibu wa Umoja wa wanawake Tanzania wilayani Kasulu, anamuona Mandela kama kioo cha afrika ambacho kilitumika kujenga hoja ya uafrika na uzalengo kwa waafrika

Chama cha mapinduzi sit u kimeshusha bendera yake nusu mlingoti bali pia viongozi wake ngazi ya taifa wanajipanga kushiriki katika shughuli za kumuenzi Mandela pamoja na kushiriki mazishi yake

Aidha viongozi hao wa chama ambacho kilishirikiana na chama cha ukombozi wa weusi wa afrika kusini ANC kuhakikisha makabulu wanaacha ubaguzi, hapa katibu wa CCM wiiaya ya Kasulu anaeleza hisia zake kuhusu kifo cha Mandela

“Mandela licha ya kuwa mpigania haki alikuwa mwenye upendo na huruma kiasi cha kuwahurumia adui zake na adui wa waafrika yaani makaburu ambao waliwanyonya na kuwanyanyasa waafrika”

Kitendo cha Mandela kuwasamehe bila kuwachukulia hatua za kisheria waliomweka gerezani kwa zaidi ya miaka 20 tena kwa uonevu pamoja na vitendo vya ubaguzi wa rangi, kulimkweza sana Mandela na kudhihirika kweli kama mkombozi wa kweli
Je Chama cha mapinduzi kinasemaje kuhusu msimamo huo wa Mandela? Bw. Minja katibu wa CCM anatanabahisa kuhusu msimamo huo wa hayati Mandela

Kwa niaba ya waandishi wa habari na wawakilishi wa channel afrika katika eneo la maziwa makuu pamoja na familia yangu tunatoa pole kwa wanafamilia ya marehemu Mandela pamoja na taifa zima la afrika kusini kwa kuondokewa na mwasisi wa ukombozi wa watu weuzi nchini afrika kusini, Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe

Kutoka Dar es Salaam kwa hisani ya Facebook, Mwanahabari Erick David anaongeza

FEBRUARY 11, 1990 BAADA YA KUACHIWA KUTOKA GEREZANI MJINI CAPETOWN,BAADA YA AWALI KULETWA HAPO KUTOKA ROBBEN ISLAND ALIKOKAA JEMA MIAKA 18 KATI YA 27 ALIYOKAA GEREZANI.MOJA YA PICHA ZA MWANZO KABISA,SIKU HII ALILALA KWA MSHIKAJI WAKE BISHOP DESMOND TUTU, KWA SIKU 2 KISHA AKAENDA KWAKE SOWETO ORLANDO WEST MTAA WA VILAKAZI, AMBAO NDIO MTAA PEKEE DUNIANI HADI SASA WALIKOISHI WASHINDI WAWILI WA NISHANI YA NOBEL,NAO NELSON MANDELA NA DESMOND TUTU.


DAFTARI LA WAPIGA KURA KUREKEBISHWA KUELEKEA KATIBA MPYA

Written By Unknown on Alhamisi, 5 Desemba 2013 | 11:23


Waziri mkuu Mizengo Pinda leo amelithibitishia Bunge kuwa Tanzania itafanya maboresho ya daftari la wapiga kura

Amesema hayo Bungeni mjini Dodoma wakati mjadala wa mswada wa marekebisho wa sheria ya mabadiliko ya katiba mpya ukielekea ukingoni

Miongoni mwa mambo ambayo yanaibuka ni suala la upigaji wa kura za maoni ambapo tume za uchaguzi Tanzania na Zanziba zitaratibu upigaji kura huo


CLOUDS FM LIVE NDANI YA KWIGIZE NEWS DOT COM




Katika kuboresha mtandao wetu wa Kwigize News and Communication Network, tumefanya maboresho makubwa ikiwa ni pamoja na kukuwekea ukurasa wa maoni

Aidha tumeungana na Clouds Media kwa kukuwekea matangazo ya moja kwa moja ya Clouds FM katika mtandao huu wa kijamii (blog)

Matangazo ya clouds fm sasa yanasikika moja kwa moja kupitia katika blog ya kwigizenews,com live bila chenga, fungua angalia mkono wa kulia fungua kitufe kisa sikiliza clouds fm kwa raha zako.


Tumeboresha bia kwa kukuwekea ukurasa wa kujiunga ilii uweze kupata habari kupitia katika ukurasa wa barua pepe yako yaani e-mail

Tunakushukuru sana kwa kututembelea na tunakualika kuleta maoni zaidi ili tuweze kuboresha zaidi


 
Shukrani kwa : Harold Dickson | Prosper Kwigize | 0752490120
Copyright © 2013. KWIGIZE NEWS AND COMMUNICATION - Haki zote zimeifadhiwa
Email us: kwigizenews@gmail.com
0764243377