Ukosefu wa
ajira ni changamoto kubwa duniani kote. Hili linasikitisha kwa kuwa kazi ni
chanzo cha heshima binafsi, amani na utulivu.Tanzania, miongoni mwa nchi
za dunia ya tatu, imechukua hatua muhimu katika kuendeleza sekta yake ya ajira,
japo bado inakabiliwa na changamoto kubwa katika hilo. Asilimia kubwa ya
watanzania wenye uwezo wa kufanya kazi, aidha hawana ajira au ajira walizonazo
haziendani na uwezo wao.
Kutokana
na ushindani mkubwa katika soko la ajira na ongezeko kubwa la vijana wanaoingia
kwenye soko la ajira (800,000 hadi 1,000,000 kwa mwaka), sekta rasmi imekosa
mafanikio katika kuzalisha fursa za ajira, hasa mijini. Matokeo yake ni;
kiwango cha umasikini kimeongezeka.
Sababu kuu
zinazochangia fursa duni za ajira ni pamoja na:
· Kutokuwa
na usawa kati ya supply ya wafanyakazi na mahitaji. Ukweli ni kwamba, supply ya
wafanyakazi ni kubwa kuliko demand ya wafanyakazi katika soko la ajira. Kila
mwaka tunashuhudia ongezeko la vijana wanaomaliza masomo yao ambao wanaingia
mtaani kuongeza idadi ya watafutao kazi.
· Vijana
kukimbilia kutafuta kazi mijini. Asilimia kubwa ya vijana wakimaliza elimu yao,
hufikiria kwenda mijini kutafuta ajira, na wengi wao huwa na mawazo ya kufanya
kazi ‘za ofisini’. Hili linasababisha shinikizo na ushindani mkubwa wa fursa za
ajira. Laiti kama vijana wengi wangeamua kujikita katika sekta ya kilimo cha
kisasa au sekta nyingine tofauti tofauti kwa kutumia elimu yao, ongezeko la
watafutao kazi mjini lingepungua kwa kiasi kikubwa.
· Elimu
duni. Hili linajumuisha kutokujua kusoma na kuandika na ukosefu wa mafunzo
sahihi yanayomuandaa mtu kuingia katika soko la ajira. Hakuna mwajiri anayeweza
kuajiri mtu asiye na stadi muhimu za kitaaluma zinazohitajika katika kazi.
Inaaminika kuwa, zaidi ya 61% ya wahitimu wanakuwa hawako tayari kiushindani
katika soko la ajira.
Kutokana
na mwangaza huo wa hali halisi ya ajira nchini Tanzania mradi wa #RecruitMe umejipanga
kusaidia kila mwenye uwezo wa kufanya kazi, vijana na wazee ili waweze kupata
ajira wanazotaka. Tunafahamu kwamba ukosefu wa kazi ni jambo linalotatiza wengi
na wengi kuhisi kuwa wamenyimwa haki yao kama binadamu ndani ya jamii
wanayoishi.
Kwa
hiyo, #RecruitMe kwa makusudi mazima imeamua
kujitolea kuweka jukwaa ambalo kila mtu anaweza kulitumia anapotafuta ajira
sahihi na kupitia jukwaa hilo, mtu anaweza kugundua fursa mpya zilizopo katika
soko la ajira. Zaidi ya hayo, waajiri wanaweza kunufaika sana kutokana na
jukwaa hili, kwa kuwa linatoa fursa kwao pia kutafuta wafanyakazi
wanaowahitaji.
Lengo kuu
la mradi huu si kuwapa watu ajira yeyote tu, la hasha, bali ni kuwapatia watu
ajira zenye hadhi, heshima na kufanya ndoto za mtu kuwa kweli. #RecruitMe itakupatia
ajira inayokubalika kisheria, yenye mapato yanayoendana na kiwango cha kazi na
ujuzi wako. Tunakuthibitishia ajira itakayojali haki zako kama mwanadamu na
mfanyakazi, ikiwa ni pamoja na kujali maslahi yako.
Ili kupata
huduma zetu, tafadhali tembelea tovuti yetu http://goo.gl/zPLquy ambapo
utakuwa na uwezo wa kuona fursa za ajira mbalimbali, pamoja na kujenga profile
yako mwenyewe. Huna haja tena ya kutokwa na jasho kutembea kutoka ofisi moja
hadi nyingine tu na kuishia kunyimwa nafasi. Pumzika, na tembelea tovuti yetu.
Tunaweza kukusaidia kupata kazi uitakayo.