HABARI MPYA
blink

HOTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA TANZANIA

Written By Unknown on Jumanne, 31 Desemba 2013 | 07:20



Hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania

JIPATIE NAKALA YA RASIMU YA PILI YA KATIBA YA TANZANIA

Rais Jakaya Kikwete akipokea Rasimu ya Katiba mpya kutoka kwa mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba mpya, jana jijini Dar es Salaam


RASIMU YA KATIBA MPYA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

RASIMU YA PILI YA KATIBA YA TANZANIA YAKABIDHIWA KWA RAIS KIKWETE

Written By Unknown on Jumatatu, 30 Desemba 2013 | 10:49

 
Jaji Joseph Sinde Warioba, mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete amekabidhiwa rasimu ya pili ya katiba mpya na tume ya katiba inayoongozwa na mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba.
Rais Kikwete amesema kuwa kazi iliyofanyika katika mchakato huo imewezesha makundi mbalimbali katika jamii kuchangia mawazo yao kupitia tume aliyoiunda ili kupata mawazo ya watanzania kuhusiana na katiba wanayoitaka.
Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein amekabidhiwa pia rasmu hiyo na kueleza kuwa kuwa wajumbe watakaoteuliwa katika bunge la katiba wanapswa kufanya kazi kwa bidii kama ilivyokuwa kwa kamati hii iliyomaliza kazi yake
Jaji mstaafu Warioba amesema rasimu hii wanayoiwasilisha ni ndefu kuliko ile ya awali iliyokuwa na ibara 240 wakati hii ina ibara 271 ikiwa ni matokeo ya tume kuzingatia maoni ya mabaraza ya katiba yaliyotoa maoni mengine mapya
Ameyataja baadhi ya mambo ambayo tume imebaini kuwa yalijadiliwa kwa hisia kali katika rasmu hiyo na ile ya awali kuwa ni suala la muungano hasa kuhusu muundo wake. Amesema wakati tume inazindua rasmi ya awali hawakupendekeza kuendelea kuwa na muundo wa serikali mbili ulihitaji ukarabati mkubwa ambao tume ilifikiri hautawezekana, hivyo mabaraza ya katiba yalitoa mapendekezo mengi yaliyoilazimu tume kufanya uchambuzi wa kina na kwamba iliwachukua muda mrefu wa tume.
Jaji Warioba amesema wananchi Zaidi ya 39,000 wa Tanzania bara waliotoa maoni yao kuhusu muungano na kati yao karibu 27,000 walizungumzia muundo na Zanzibar wananchi karibia wote waliotoa maoni walijikita katika muungano ambapo kati ya wananchi 38,000 wa Zanzibar waliotoa maoni 19,000 walizungumzia muundo wa muungano.
Tanzania bara asilimia 13 walitaka serikali moja, asilimia 24 walipendekeza serikali mbili na 61 walipendekeza serikali tatu, wakati Zanzibar asilimia 34 walipendekeza serikali mbili na asilimia 60 muungano wa mkataba ambapo asilimia 0.1 walihitaji serikali moja.
Hata hivyo Rasimu hiyo ya katiba iliyokabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imeorodhesha malalamiko 10 kwa upande wa Zanzibar na manane ya Tanzania Bara
Malalamiko matatu makubwa kwa Zanzibar ni Serikali ya Tanganyika kuvaa koti la serikali ya muungano hivyo kupunguza nguvu kwa Zanzibar,Ongezeko la mambo ya Muungano,kumuondoa Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Tanzania bara tume hiyo imeyataja malalamiko kuwa ni kuwa Zanzibar imekuwa nchi huru , ina bendera yake ya Taifa, ina serikali yake ina wimbo wake wa taifa na imebadili katika yake ili itambulike kama nchi wakati Tanzania bara imepoteza utambulisho wake, wananchi wa Tanzania Bara kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi Zanzibar wakati wenzao wanamiliki Tanzania bara.

RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI, JOTO LA UWAZIRI LAPAMBA MOTO

Written By Unknown on Ijumaa, 27 Desemba 2013 | 10:46

Rais Jakaya Kikwete amewsaili nchini leo akiwa na lake moyoni kuhusu hatima ya baraza lake la mawaziri, baada ya kutengua uteuzi wa mawaziri wake wanne, wiki mbili zilizopita.
Rais Kikwete alikwenda Marekani, Desemba 18, mwaka huu kufanyiwa uchunguzi wa afya yake na akiwa huko, upepo wa kisiasa ulibadilika na kumlazimisha kuchukua hatua hiyo ambayo inampa wajibu wa kupanga upya safu yake ya uongozi.
Mawaziri ambao uongozi wao ulitenguliwa ni wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi, Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, Dk Mathayo David Mathayo.
Kung’oka kwao kunatokana na ripoti ya kamati ndogo ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kuhusu athari zilizotokana na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili, ambayo ilizua mjadala mkali kiasi cha wabunge kumshinikiza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwamba naye aachie ngazi.
Hivyo kitendawili kingine kikubwa kinachomkabili Rais Kikwete ni iwapo ataamua kuendelea kufanya kazi na Pinda ambaye alishambuliwa na wabunge kwamba naye ang’oke kwa madai kwamba ameshindwa kusimamia utendaji serikalini.
Kwa mujibu wa Katiba ya nchi, Ibara ya 52(1) Waziri Mkuu ndiye mwenye madaraka juu ya kudhibiti usimamiaji na utekelezaji wa siku wa kazi na shughuli za Serikali.
Katiba inasema: “Katika utekelezaji wa madaraka yake, Waziri Mkuu atatekeleza au kusababisha utekelezaji wa jambo lolote au mambo yoyote ambayo Rais ataagiza kwamba yatekelezwe. Ibara ya 53 (1) inaeleza: “Bila kuathiri masharti ya Katiba hii, Waziri Mkuu atawajibika kwa Rais kuhusu utekelezaji wa madaraka yake.”
Hata hivyo, ni kama Rais Kikwete alishaamua kumwokoa Pinda pale alipompa maagizo kwamba alitangazie Bunge uamuzi wake wa kutengua uteuzi wa mawaziri wanne.
Ripoti hiyo iliyosomwa na Mwenyekiti wake, James Lembeli ilifichua kuwapo kwa vifo na mateso ya wananchi vilivyofanywa wakati wa operesheni hiyo iliyoendeshwa na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), maofisa wa Usalama wa Taifa na Polisi.
Mbali ya pengo lililoachwa na mawaziri hao wanne, Rais Kikwete pia ndiye mwenye majawabu kuhusu hatima ya wale waliotajwa kuwa ni mawaziri mizigo kwa kushindwa katika utendaji wao, hasa ikizingatiwa kuwa shinikizo la kuwajibishwa kwao linatoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho yeye ni mwenyekiti wake.
Kitendawili cha Pinda
Zipo hoja kadhaa, iwapo Rais Kikwete atamwondoa Pinda kama ambavyo wabunge walisisitiza wakati wakichangia ripoti hiyo, huku wakirejea yaliyowahi kutokea serikalini lakini Waziri Mkuu huyo akakwepa kuwajibika.

SUDANI KUSINI HALI TETE, RAIS UHURU NA HAILE WAENDA KUNUSURU

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn(kushoto) Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini(katikati) na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya(kulia)wakiwa mjini Juba 

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya hapo jana walikutana na Rais Salva Kiir mjini Juba na kusema kwamba wamepiga hatua nzuri za maendeleo kwa kwa kile walichokitaja kuwa mazungumzo ya amani. Viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali ya Kanda IGAD wanatarajiwa kukutana mjini Nairobi leo hii kuendeleza juhudi za kukomesha mzozo wa umwagaji damu wa kikabila unaopamba moto Sudan Kusini.
Hali ya mvutano katika nchi hiyo iliojipatia hurun wake kutoka Sudan miaka miwili tu iliopita ilikuja kuripuka kuwa mzozo wa umwagaji damu hapo Disemba 15 kwa mapambano makali kati ya vikosi vilivyo tiifu kwa Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na vile vinavyomuunga mkono makamo wake Riek Machar aliyetimuliwa madarakani. Mapigano hayo sasa yamezagaa hadi kwenye majimbo kumi ya nchi hiyo.
Juhudi kukomesha umwagaji damu
Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini(UMINSS) wakiwa katika doria kwenye eneo lao kwenye viunga vya Juba.
Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini(UMINSS) wakiwa katika doria kwenye eneo lao kwenye viunga vya Juba.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo Jumanne limekubali kuongeza takriban maradufu ukubwa wa kikosi chake cha kulinda amani kinachojulikana kama UNMISS ili kuweza kufikia wanajeshi 12,500 na polisi 1,300 baada ya mzozo huo kuonekana kushindwa kudhibitika.
Wakati jumuiya ya kimataifa ikiwa mbioni kuizuwiya nchi hiyo kutumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe Umoja wa Mataifa hapo jana umetangaza kwamba vikosi vya ziada na zana muhimu za kijeshi kama vile helikopta zitakuwa zimewekwa nchini humo kufikia hapo kesho.
Hilde Johnson ni mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Sudan Kusini amesema wanaongeza wafanyakazi wao kwenye maeneo muhimu yanaohitaji usalama na kuimarisha kambi zao zinazohitaji kuimarishwa kijeshi.Amesema hiyo ina maana kwamba wanahamisha wanajeshi wao wa kulinda amani kutoka maeno ambayo hivi sasa hayana umuhimu na kuwapeleka kwenye kambi zao za Juba,Bor na Bentiu.
Mapambano yanaendelea
Familia zilizopoteza makaazi zikiwa kwenye kambi ya Umoja wa Mataifa huko Jabel kwenye kiunga cha mji mkuu wa Juba.
Familia zilizopoteza makaazi zikiwa kwenye kambi ya Umoja wa Mataifa huko Jabel kwenye kiunga cha mji mkuu wa Juba.
Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini Philip Aguer ameliambia shirika la habari la AFP kwamba vikosi vyake vinapambana na vikosi vyenye kumuunga mkono Machar ndani ya mji wa Malakal ambao ni mji mkuu wa jimbo la Upper Nile.Pia amesema vikosi hivyo vinajiandaa kuushambulia mji wa Bentiu mji mkuu katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Unity.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa maelfu ya watu wameuwawa na zaidi ya watu 120,000 wamepotezewa makaazi kutokana na kuendelea kwa mzozo huo wa umwagaji damu ambapo nusu yake wanatafuta hifadhi kwenye kambi za Umoja wa Mataifa nchini humo. Huku kukiwa na repoti za maiti kuzikwa kwenye makaburi ya pamoja na ushahidi wa watu kunyongwa na kubakwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameahidi wale waliohusika na vitendo hivyo watawajibishwa.
Mwandishi: Mohamed Dahman/AFP/AP
Mwandishi:Abdul-Rahman

DRC KWANUKA TENA WANANCHI WAUWAWA

Siku chache baada ya serikali ya DRC kuingia mkataba wa amani na wapiganaji wa M23 ambao wanatajwa kutaka kugeuza kundi lao la vijeshi kuwa chama cha siasa, kundi jingine linalotajwa kuwa la Raia wa Uganda limefanya mashambulizi dhi ya raia mashariki mwa DRC

Hata hivyo imeelezwa kuwa majeshi ya serikali kwa msaada wa kikosi cha jeshi la umoja wa mataifa limefanikiwa kuwadhibiti na kuwakimbizi wanajeshi hao wa kikosi cha uasi

Msemaji wa shirika la Kimataifa la Msalama Mwekundu ICRC, amesema waliojeruhiwa wamepelekwa Goma kwa matibabu.

Amesema shirika la msalaba mwekundi nchini Congo linaendelea na shughuli ya kusaidia katika harakati za kuwazika waliouawa kwenye mapigano hayo.

Jeshi la Congo lina kambi mjini Kamango ambalo limekuwa likishambuliwa na wanamgambo wa waasi mara kwa mara, wakiwemo waasi wa Kiislamu kutoka Uganda wanaohudumu nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

SALAAM ZA NOELI NA MWAKA MPYA

Written By Unknown on Jumanne, 24 Desemba 2013 | 12:23


Kampuni ya PLEN Media and Entertainment Network kwa pamoja na mtandao wa  Kwigize News tunawatakia wasomaji wetu wote heri ya sikukuu ya Kuzaliwa kwa YESU Kristo Iwe siku ya amani na furaha kwenu, aidha tunawatakiwa heri na baraka tele wakati wa kuupokea na kuuishi mwaka mpya

PLEN Media and Entertainment Tunatarajia kuwa mwaka 2014 utakuwa mwaka wa mafanikio, na tunatarajia kusajili kituo kipya cha RADIO kitakachojulikana kwa jina la PLEN RADIO FM KASULU Radio hii itakuwa ni mkombozi kwa vijana, wazee na akina mama kwakuwa malengo yake yatakuwa kwa ajili ya kubadili fikra za jamii katika maendeleo

MUNGU AWE PAMOJA NASI SOTE

AMINA

ZITTO AMLIPUA MBOWE -POSHO ZA BUNGE NA MASHANGINGI

Written By Unknown on Jumapili, 22 Desemba 2013 | 10:11


Mbunge wa Kigoam Kaskazini Zitto Kabwe amelipua kwa wananchi Mwenyekiti wake wa Taifa Freeman Mbowe kwa kukiuka taratibu na kanuni za Bunge kwa kujipatia fedha za kazi za Bunge na kisha kuzitumia kwa anasa

Hayo yametajwa na Zito Kabwe wakati akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Kasulu akijibu hoja za kamati kuu kumvua madaraka yake ya kichama

Zitto amesisitiza kuwa viongozi wake wa chama wanajaribu kuyumbisha hoja muhimu kama vile, kuchukua fedha za bunge na kwenda kutanua, kukataa mahesabu ya chama kukaguliwa, kuchukua mashangingi na kupokea posho kinyume na makubaliano na kanuni za chama chao.

amesisitiza kuwa kamwe hata kaa kimya na kwamba ataendelea kupinga jambo lolote ambalo linaenda kinyume na maadili ya CHADEMA na hataondoka katika chama hichou licha ya kuwepo kwa shinikizo kubwa

"chama chetu tumehangaika kukijenga, sasa wapo wambao waliingia kwa hiyari CHADEMA na wapo ambao walifukuzwa CCM, au walikosa kura za Maoni CCM ndipo wakaja katika chama chetu na hao ndio wanataka wao waonekane wanakijua chama na wana uchungu nacho kuliko sisi tulioingia kwa hiyari na mapenzi yetu kwa demokrasia" alisisitiza Kabwe

Ikumbukwe kuwa Katibu mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa kabla ya kujiunga na chama hicho alikuwa mgombea wa CCM na alikimbilia huko baada ya kushindwa katika kura za maoni katika uchaguzi wa ndani ya CCM Jimbo la Karatu

ZITTO KABWE ASISITIZA HANG'OKI CHADEMA, ASHUTUMU SLAA NA MBOWE KWA UBABAISHAJI

Sehemu ya wananchi wa mjini Kasulu waliojitokeza kusikiliza hotuba ya zito kabwe ambayo sehemu kubwa ilihusu kupinga kuvuliwa madaraka ndani ya chama chake pamoja na kuwataka wananchi kuungana kuwapinga viongozi wa Kamati kuu ya CHADEMA iliyowavua uongozi Zitto Kabwe, Dr. Kitilya Mkumbo na Migamba kwa tuhuma za Uhaini na usaliti kwa chama hicho
ZITTO KABWE aliyekuwa Naibu Katibu mkuu na naibu msemaji wa Kambi ya Uoinzani Bungeni (aliyevaa nguo za asili) Muda mfupi baada ya kuvalishwa mavani ya kitemi na wazee wa Heru juu katika JImbo la Kasulu Mjini, kabla ya kuanza kuwahutubia maelfu waliofurika uwanjani hapo. Mkutano huo uliandaliwa na kundi la viongozi wa CHADEMA jimbo ambao pia hivi karibuni wamefukuzwa uongozi na chama hicho ngazi ya wailaya kwa kile kinachotajwa kuwa ni kumuunga mkono ZItto na kupinga uamuzi wa kamati kuu

Viongozi wa Chadema kadhaa hasa wa ngazi za juu wilaya ya Kasulu hawakujitokeza katika mkutano huo.
Maelfu ya wakazi wa Mji wa Kasulu mkoani Kigoma wakimsikiliza mbunge wa Kigoma Kaskazini (aliyefukuzwa unaibu katibu mkuu wa Chadema) wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja ambapo Dr. Slaa alishambuliwa na wananchi wanaopinga kamati kuu ya chama hicho kumfykuza uongozi ZITTO


WABUNGE WA UPINZANI WATAJWA KUULIZA MASWALI NA HOJA ZA KUTUMWA BUNGENI

Wabunge wakiwa katika vikao Bungeni

Na. Mwandishi wetu
Dodoma

Imebainika kuwa baadhi ya wabunge wa majimbo hawna uwezo wa kujenga hoja wala kusimamia jambo lolote bungeni, wawapo katika vikao inapoibuka hoja yoyote hutegemea wabunge wenzao kuwaandalia maswali au kuwashinikiza kuuliza maswali hasa yanayolenga kuihujumu serikali.

Hayo yemebainika pia katika kikao cha Bunge siku ya ijumaa December 20 wakati wa kujadili taarifa ya kamati ya kudumu ya ardhi maliasili na mazingira iliyokuwa ikijadili kuhusu ukiukwaji wa miongozo wakati wa operesheni Tokomeza, Baadhi ya wabunge wakiwemo wa mkoa wa Kigoma waliuliza maswali ya kutumwa au kutungwa na wenzao na wao kuwa vipaza sauti tu.

Je kwa karne hii ya sayansi na teknolojia Bado Tanzania inahitaji wabunge ambao wao hawana la kuliambia taifa hadi washawishiwe au wahinikizwe na wabunge wenzao? Je Upinzani tunaopigania kuujenga ili kupambana na CCM unajengwa kwa njia ya mashinikizoo na maswali ya kuongozwa na wengine

TAFAKARI CHUKUA HATUA

ZITTO KABWE APOKELEWA KIGOMA KAMA LULU

Written By Unknown on Jumamosi, 21 Desemba 2013 | 12:23

Sehemu ya Umati wa maelfu ya wananchi na mashabiki wa chama cha demokrasia na maendeleo wakimsikiliza mbunge wa \kigoma kaskazini aliyefutwa uongozi ndani ya CHADEMA.
Picha na Fadhil Abdalla, Kigoma

Siku chache baada ya Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendelo Dr. Wilbroad Slaa kufanya ziara iliyokumbwa na vikwazo vya kutokukubalika kwa wananchi, fujo, maandamano, mabango na kurushiwa mawe akipingwa  kutokana na kamati kuu ya chama hicho kumfukuza uongozi Zito kabwe, hali imekuwa kinyume kwa mbunge huyo anapoingia mkoani kigoma

Hayo yametokea leo ambapo magari, pikipiki, umati mkubwa wa watu wakubwa kwa wadogo wakiandamana kutoka uwanja wa ndege wa kigoma hadi viwanja vya mwanga centre ambapo amehutubia na kusikilizwa kwa utulivu mkubwa

Kesho Kabwe atazuru wilaya ya kasulu ambako Dr. Slaa alipigwa mawe na kuzomewa na hatimaye kushindwa kuhutubia wananchi baada ya gharika la mawe lililofuatwa na jeshi la polisi kurusha mabomu ya kutoa machozi na mkutano kuvunjika


BREAKING NEWS........MAWAZIRI WANNE TANZANIA WATUPWA NJE MMOJA AJIUZURU

Written By Unknown on Ijumaa, 20 Desemba 2013 | 11:11

Blozi hamis Kagasheki aliyekuwa \waziri wa Maliasili na Utalii

Waziri wa mali asili na Utalii Balozi Kagasheski, jioni hii ameamua kujiuzuru kufuatia shinikizo kubwa la wabunge waliokuwa wakiijadili taarifa ya uchunguzi wa operesheni Tokomeza iliyokuwa ikidhamilia kutokomeza ujangiri dhidi ya wanyama pori hususani Tembo (Ndovu)

Kagasheki ni miongoni mwa mawaziri wanne waliotuhumiwa na kamati ya bunge ya ardhi maliasili na mazingira waliosababisha uzembe na kutokea kwa mauaji na udharirishaji wakati wa operesheni tokomeza

Iadaiwa kuwa waziri wa Ulinzi, \waziri wa mambo ya ndani na waziri wa Mifugo na uvuvi nao Rais w=amewachukulia hatua

CHAMA CHA HAYATI PATRICE LUMUMBA CHAILAUMU RWANDA NA UGANDA

Hayati Patrice Lumumba 
Chama cha MNC Lumbumba kilichopigania uhuru wa DRC iliyokuwa ikijulikana kama Zaire chini ya Hayati Patrice Lumumba, kimeituhumu nchi ya Rwanda na Uganda kwa kujaribu kuimega nchi ya jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na kuunga mkono vikundi vya uasi vya M23

Katibu mkuu wa chama hicho Bw. Venance Wialango amebainisha hayo katika mahojiano na Channel Africa jijini Dar es salaam na kubainisha kuwa tangu kuuwawa kwa Patrice Lumumba DRC imekuwa ikivamiwa na Rwanda kwa kusapoti wapambanaji wanaojiita wapigania uhuru

Amesisitiza kuwa vikosi vya uasi vinavyojikita mashariki mwa DRC hususani mikoa ya KIVU ni vinavyoundwa na wanyarwanda na kupewa msaada na serikali ya Rwanda na Uganda

Amesisitiza kuwa waasi hao hawana nia na amani ya DRC zaidi ya kutumia uasi huo kuvuna mali hususani madini yaliyosheheni katika eneo la Kivu Kusini na Kaskazini kwa kisingizio cha kutaka kuingizwa katika serikali ya Joseph Kabila

Akizungumzia kuhuru kikundi cha M23 na mahusiano yake na Rwanda Bw. Wialango amesema ni masalia ya vikosi vya Rwanda vilivyomsaidia Hayati rais Laurent Kabila ambao hawakuingizwa katika jeshi la serikali

“Katika harakati za kumwondoa Rais Mobutu Madarakani, Laurent Kabila alitumia wapambanaji wa aina nyingi miongoni mwao walikuwa ni hao Wanyarwanda walioko katika misitu ya Kongo na makubaliano yalikuwa ni baada ya kuchukua nchi wao wangerejea makwao, sasa hali ikawa kinyume, wakasisitiza kuingizwa katika Jeshi la taifa, alipokataa killichotokea ni kuuwawa” anasema Wialango

Aidha Katibu huyo mkuu wa chama cha MRC Lumumba Bw. Venance ameipongeza Tanzania kwa kuongoza jeshi la umoja wa mataifa chini ya vikosi vya SADC kuwaondoa wapiganaji wa M23 mashariki mwa kongo na kusisitiza kuwa ipo hata ya mataifa kuamini kuwa Rwanda ndiyo inayowapa nguvu wapiganaji hao

Hata hivyo ameelezea kusikitishwa na kitendo cha Rais Kabila kuingia mkataba na M23 ambao wameshindwa katika vita, na kwamba kitendo hicho kinachochea hisia kuwa Kabila naye ni mfadhili wa uasi huo mashariki mwa DRC


MAHAKAMA YA MAUAJI YA KIMBARI YA RWANDA ICTR ARUSHA YALAUMIWA KWA UBAGUZI



Kiongozi wa chama cha upinzani cha Ukombozi wa Wanyarwanda ULDR nchini

Rwanda Bw. Hakiza Pauline ameitupia lawama mahakama ya kimataifa
inayoshughuikia mauaji ya kimbali ya Rwanda ICTR iliyoko mkoani Arusha
kwa kuendesha shughuli zake kwa mlengo wa ukabila

Akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar salaam ambapo
yupo kwa ajili ya kusaka uungwaji mkono, Hakiza ambaye anishi
uhamishoni nchini Afrika kusini, amesema ICTR imekuwa ikiwaandama
wahutu pekee kwa tuhuma za mauaji ya watusi na kuongeza kuwa, vita vya Rwanda vya mwaka 1994 vilihusisha makabila yote


Pamoja na madai hayo ya Hakiza wa chama cha ULDR, kwa upande wake
mahakama ya ICTR imekanusha vikali madai hayo na kusisitiza kuwa
hakuna upendeleo wa kikabila katika usikilizaji wa kesi

Mkuu wa kitengo cha habari cha mahakama hiyo Bw. Danford Mpumilwa
ameiambia channel Africa kuwa hizo ni hisia za kibinadamu, katika line
ya simu Danford mpumilwa tuambie kuna ukweli wa madai hayo ya ubaguz
na ukabila mahakamani hapo


Bw. Mpumilwa amekanusha madai hayo na kusisitiza kuwa mahakama hiyo inazingatia sheria za kimataifa za makosa ya jinai na hakuna vitendo vya ubaguzi katika mahakama hiyo.

MEDIA COUNCIL SEASON GREETINGS TO ALL M C T MEMBERS

Written By Unknown on Jumatano, 18 Desemba 2013 | 01:56


MKATABA WA SERIKALI YA DRC NA KIKUNDI CHA M23 WAPINGWA

Written By Unknown on Jumanne, 17 Desemba 2013 | 22:41

Kushoto ni Bw. Prosper Kwigize mwandishi wa habari wa shirika la utangazaji la Afrika Kusini SABC/Channel Africa akifanya mahojiano na Bw. Venance Wialango ambaye ni Katibu mkuu wa chama kilichopigania Uhuru wa Zaire (DRC) MNC/Lumumba 

Siku chache baada ya Rais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila kusaini mkataba wa amani na kikundi cha waasi cha M23 katika hafla iliyohudhuriwa na marais Yoweli Museveni wa Uganda na Joyce Banda wa Malawi jijini Nairobi, Raia wa kongo walioko Tanzania pamoja na viongozi wa vyama vya upinzani nchini DRC wamepinga mkataba huo

Wakiongea na channel africa kwa nyakati tofauti raia hao wametaja kuwa M23 hawakupaswa kuingia mkataba wa aina yoyote na DRC kwa kuwa ni kikundi kilichoshindwa katika vita na kwamba tangu awali hawakuhitaja suluhu

Venance Wialango Katibu Mkuu MNC Lumumba
Venance Wialango ni katibu mkuu wa chama cha MNC/Limumba anayeishi uhamishoni nchini Tanzania hapa anasisitiza kuwa M23 wameshinda vita na hawakuwa tayari kuingia mkataba wowote na serikali ya Joseph kabila kabla ya kupigwa kijeshi na majeshi ya SADC chini ya dhamana ya umoja wa mataifa

Kwa upande wao wakimbizi kutoka DRC walioko Tanzania nao wamekuwa na maoni hasi juu ya mkataba huo huku wakiwatuhumu kuwa M23 ni raia wa Rwanda na Uganda wanaojaribu kuikalia nchi yao

Kutokana na mkataba huo, wakimbizi wamesisitiza kuwa hawatarejea nchiini mwao kama Rais Kabila ataendelea kuwaruusu wanyarwanda kuingia katika jeshi la taifa pamoja nakuacha wageni kuyakalia maeneo na ardhi ya DRC


Mkataba wa amani baina ya serikali ya DRC na waasi wa M23 ulisainiwa jijini Nairobi baada ya ule wa awali uliokuwa usainiwe jijini Kampala kukwama

Wakimbizi wa DRC wakiwa katika mstari kwa ajili ya kupokea mgao wa chakula katika kambi yao iliyoko wilayani Kasulu Mkoani Kigoma, Kambi hiyo ya nyarugusu ina takribani wakimbizi 65, 000 wote wakitokea mashariki mwa DRC ambako mapigano baina ya M23 yamekuwa yakiendelea kabl aya kuvulumshwa na majeshi ya Umoja wa mataifa yaliyoongozwa na Tanzania

MAPINDUZI SUDAN KUSINI YAKWAMA, WANAJESHI NA RAIA LUKUKI WAPOTEZA MAISHA


Wanajeshi zaidi ya sitini wameripotiwa kupoteza maisha katika mapambano ya uso kwa uso kati ya majeshi ya serikali na ya waasi waliotaka kuipindua nchi hiyo

Wakati huohuo afisa mmoja wa serikali amesema kuwa raia 26 wameuawa katika mapigano ya siku mbili mjini Juba.

Zaidi ya watu miamoja wamejeruhiwa huku maafisa wakuu wakijaribu kudhibiti mji huo kufuatia kile ambacho serikali ilisema ni jaribio la mapinduzi mbalo liliweza kutibuliwa.

Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini Barnaba Marial Benjamin amesema kuwa vikosi vya usalama vinawasaka wanajeshi watiifu kwa Riek Machar aliyekuwa makamu wa Rais wa Salva Kiir anayedaiwa kupanga njama hiyo ya mapinduzi.

Taarifa zinasema kuwa milio ya risasi ingali inasikika mjini Juba huku wanasiasa kumi wakikamatwa kuhusiana na njama hiyo ya mapinduzi.

DO YOU KNOW THIS, A HUGE NUMBER OF MIGRANTS HAS DIED THIS YEAR


DECEMBER 17 INTERNATIONAL DAY FOR MIGRATION

17 December 2013
It’s Time to Take Action and Save Lives of Migrants Caught in Crisis EN | FR | ES
It’s Time to Take Action and Save Lives of Migrants Caught in Crisis
William Lacy Swing IOM Director General
International Migrants Day 2013

Geneva 17 December 2013 - The International Organization for Migration warns today that unless the international community takes decisive action to address the causes of irregular migration, more migrant lives will be lost at the hands of people smugglers and traffickers. 
Observing International Migrants Day (18 December) the Organization’s Director General, William Lacy Swing noted that 2013 may have been the costliest year on record in terms of lives lost, for migrants seeking to cross international borders clandestinely.
“We will never know the true total, as many migrants died anonymously in deserts, in oceans or in other accidents,” stated Ambassador Swing.  "However, our figures show that at least 2,360 migrants died this year while chasing the dream of a new life. These people are desperate – not even a very real fear of death prevents them from making their journey.”
The Mediterranean island of Lampedusa, the Caribbean, and the seas off Thailand and Indonesia have all seen tragedies involving overloaded, un-seaworthy vessels going down resulting in the deaths of dozens of migrants per episode.
The US Mexico border area and the desert route from West Africa to Libya are the most dangerous land routes, with migrants perishing in train accidents, murdered, or dying of thirst in their quest for a better life.
“On this International Day we focus on the well-being and safety of migrants. IOM calls for strengthening existing policies or developing new ones to protect the human rights of those who leave home to seek better opportunities. We are ready to assist our Member States and other partners in the development and implementation of policies.”
Mr. Swing warned that the doors of previously-welcoming countries are increasingly being shut on the poorest, most desperate migrants. IOM has observed a direct link between tighter border controls and increases in people smuggling, which is now a US35-billion dollar a year business.
“It’s time to take action and save the lives of migrants who would otherwise die while taking desperate measures to cross increasingly restrictive borders. We are calling for measures to enable employers in countries with labour shortages to access potential migrants to work and we need to ensure that these people are not exploited or exposed to gender based violence.
“We need a whole-of-government, whole-of-society approach in the best interests of countries, communities and people, in particular migrants themselves,” continued Mr. Swing.
Conflict and natural disasters are adding to the number of people on the move.  Some 5,000 people a day left the Central Philippines following typhoon Haiyan last month. A further 100,000 fled fighting in the Central African Republic in the first half of December.
In 2016 there will be a World Humanitarian Summit: IOM will be asking how the global humanitarian community can ensure that political upheaval, economic stress and natural calamities do not always lead to a second round of challenges whereby migrants feel forced to take desperate measures. 
 The full figures, trends and analysis will be captured in a report to be issued by IOM.

IJUE AZAM TV, INAYOTOA HUDUMA YA KISASA NA KUMUWEZESHA MTUMIAJI KUREKODI MATANGAZO

Kulia katika picha ni Rhys Torrington: Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd
Habari zimeandikwa na Khadija Mahamba na Lucy Ngongoseke
Dar es Salaam

Huduma za matangazo ya AzamTV zilianza kupatikana hewani Kuanzia Ijumaa Desemba 6, 2013 kwa kuwawezesha wateja waliounganishwa kwenya kisimbuzi kungalia bure hadi hii leo ambapo huduma kwa malipo inaanza rasmi kwa ada ya shilingi 12,500 kwa mwezi.

Kwa kuanzia huduma ya AzamTV itahusisha chaneli 50 zinazojumuisha chaneli maarufu za kimataifa, chaneli maarufu za ndani na chaneli tatu maalumu za Azam ambazo ni:
·         Azam One – burudani kwa familia kutoka Afrika, sehemu kubwa ya matangazo   itakuwa kwa lugha ya Kiswahili.
·         Azam Two – vipindi maalum kutoka sehemu mbalimbali za dunia 
·         SinemaZetu – Chaneli maalumu kwa tamthilia za kitanzania kwa saa 24.
Kwa pamoja, chaneli tajwa zitawapa wateja wigo mpana wa kufaidi matangazo bora ya michezo, tamthilia, watoto na maisha.

Kundi la T-Afica likituwa burudani wakati wa ufunguzi wa ofisi ya AZAMTV siku ya jumatatu tarehe 16 Desemba 2013
Ofisi ilifunguliwa rasmi na Bw. Yusuf Bakhresa: Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Ltd.

“Ofisi hii ya makao makuu ambayo kwa hakika ni ya kuvutia ni kielelezo cha nia thabiti ya Azam Media kufanya kazi kwa umakini katika shughuli ya utangazaji hapa Tanzania. Dira yetu ni kutoa burudani ya kiwango cha juu kwa familia kwa bei nafuu kote nchini, na baadaye kote barani Afrika. Hili ni jambo ambalo kila mmoja hapa nchini anapaswa kujivunia.” Alisema Bakhresa

Rhys Torrington: Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd alisema: “Naona faraja kubwa kwamba leo hii AzamTV  ipo sokoni kwa ajili ya kila mtanzania. Tutahabarisha, kuelimisha na zaidi ya yote tutaburudusha watu kote nchini. Huduma yetu inapatikana kwa watu wote – situ katika ofisi hizi lakini pia kupitia mtandao wetu unaohusisha zaidi ya mawakala 50 katika kila mkoa. AzamTV ni ya kudumu”

Azam Media pia inawekeza katika utayarishaji wa vipindi vipya kupitia kampuni yake tanzu, Uhai Productions, kwa kushirikiana na watayarishaji wa vipindi wa hapa Tanzania.

Azam Media Ltd. Ni kampuni tanzu ya kundi la makampuni ya Salim Said Bakhressa (SSB).

Azam TV, ni warushaji wa matangazo ya satelaiti kwa mfumo wa digiti ambayo itawapatia wateja wake burudani ya kiwango cha juu kwa familia kwa bei moja nafuu. Makao Makuu yapo Dar es Salaam, Tanzania amabako ilianzishwa mwaka 2013 malengo yakiwa kusambaa katika  nchi nyingine za Afrika hapo baadaye.

Dira ni kuwa na vipindi tofauti vya kimataifa na pia vya ndani ya nchi  vifaavyo kwa familia, wapenzi wa michezo na watanzania wote wa rika mbalimbali.


Watazamaji wanaweza pia kurekodi wakati wa kuangalia kwa kutumia USB. Ni utaratibu wa kawaida kwamba kisimbuzi kinakuja  na na sehemu ya kuunganisha kwa mfumo wa HDMI ili kupokea  picha ang’avu kwenye luninga.

AZAM TELEVISION BURUDANI KWA WOTE YAPATA BARAKA RASMI

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Azam Media,Yussuf Bahresa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Televisheni yao ya Azam kwenye makao makuu yao yaliopo Pugu Road,jijini Dar es Salaam wiki hii


Runinga mpya nchini Tanzania Azam TV Burudani Kwa wote imezinduliwa rasmi jijini Dar es salaam tayari kwa ajili ya kuanza kazi za mawasiliano ya habari na kusaidia jamii kujua na kupata habari za matukio mbali mbali

Akizindua Runinga hiyo mkurugenzi wa wa kampuni ya AZAM MEDIA Bw. Yusuph Bakhresa amesema matarajio ya kampuni yake ni kuifikia jamii ndani na nje ya nchi

Azam Tv imeanza kutoa huduma hivi karibuni kwa kurusha moja kwa moja mashindano ya mpira wa mguu ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania VPL na kupata mafanikio makubwa

Imeelezwa kuwa Azam TV itakuwa ikionekana katika mfumo wa Digital na kuonekana nchi nzima pamoja na nchi mbalimbali barani Africa hususani za afrika mashariki na kati 

WAGOMBEA URAIS 2015 WAHAHA KUHUSU KATIBA MPYA, WAHOFIA KUCHELEWA

Written By Unknown on Jumatatu, 16 Desemba 2013 | 11:10

Ibrahim Lipumba Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF, amekuwa akigombea Urais tangu mfumo wa vyama vingi uanze nchini Tanzania

Mchakato wa katiba mpya licha ya kuwa jambo muhimu kwa watanzania na mstakabali wa taifa, mwenendo wa wanasiasa kulalama, kuchangia, kuhimiza wananchi kuunga mkono na wakati mwingine kupinga kumekuwa kukionesha kuwa ipo haja ya kuharakisha kupatikana kwa katiba hiyo

Haraka na mihemko ya wanasiasa hususani wale ambao wamekuwa wakigombea Urais, wenye nia ya kugombea pamoja na viongozi wa vyama vya siasa, kunadhihirisha kuwa harakahraka ya kupatikana kwa katiba mpya kunalenga uchaguzi ujao na si kupata katiba makini ya Tanzania
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba amesema mchakato wa Katiba Mpya una vikwazo vingi na kwamba Katiba haiwezi kupatikana mwaka 2014 kama Rais Kikwete alivyoahidi hivyo, kuna haja ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Bara.
Hii ni mara ya pili kwa Lipumba kutoa kauli hiyo. Mei mwaka huu, alitoa tamko kama hilo alipoonyesha wasiwasi wake kuhusu upatikanaji wa Katiba Mpya akadai ni janja ya CCM kumwongezea muda Rais.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Lipumba alisema kuwa amekuwa akiutafakari kwa kina mchakato wa Katiba Mpya kama unaweza kukamilika mwaka 2014, lakini jibu linalomjia, hakuna.
Alitaja baadhi ya vikwazo ambavyo vinaweza kukwamisha kupatikana kwa Katiba Mpya kuwa ni Daftari la Kudumu la Wapigakura kama halijaboreshwa na kasi ndogo ya utoaji wa vitambulisho vya utaifa ambavyo vitatumika kupigia kura hiyo.
Wakati Profesa Lipumba akisema hayo, tayari Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imeeleza kuwa haina mpango kwa sasa wa kuboresha Daftari la Kudumu Wapigakura kwa ajili ya kura za maoni kwa sababu muda uliobaki ni mfupi.
Mwenyekiti wa Nec, Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita, kuwa itakuwa vigumu kuliboresha daftari hilo kwa ajili ya upigaji wa kura za maoni utakaofanyika mwanzoni mwa mwaka 2014 kwa sababu muda uliobaki ni mfupi na hakuna fedha za kufanya hivyo.

UJERUMANI WAUNDA SERIKALII YA MSETO

Viongozi wa serikali ya Mseto, Katikati ni Angela Markel aliyeshinda katika uchaguzi uliomalizika hivi karibuni

Kwa mara ya kwanza katika historia chama cha upinzani cha SPD ambacho kilishindwa katika uchaguzi mkuu wa Ujerumani uliofanyika hapo mwezi wa Septemba kiliwataka wanachama wake wapige kura kuridhia chama hicho kujiunga katika serikali ya mseto chini ya uongozi wa Kansela Angela Merkel

Chama cha Angela Merkel kilishinda katika uchaguzi mkuu huo.Matokeo ya kura hiyo ingelikuwa ya "hapana" ingelibidi kufanyike mazungumzo mapya ya kuundwa kwa serikali hiyo ya mseto.

Katika ngazi ya kitaifa ya serikali ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kulikuwako mara mbili kwa serikali za muungano mkuu.Kwa mara ya kwanza serikali hiyo iliundwa kati ya vyama ndugu vya CDU/CSU na chama cha SPD hapo mwaka 1966.

Mara ya pili serikali hiyo ya muungano mkuu iliundwa hapo mwaka 2005 hadi 2009 na kuungozwa na Kansela Angela Merkel.


SANAMU YA MANDELA YATAWALA DUNIA KWA UKUBWA WAKE


Siku moja tu baada ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa kwanza mweusi na mpigania Uhuru wa Africa kusini Nelson Mandela, Sanamu kubwa zaidi duniani inayomuonesha akihamasisha umoja na maridhiano imezinduliwa katika mji mkuu wa Afrika kusini Pretoria

Sanamu hiyo iliyotengenezwa kwa shaba ina urefu wa mita tisa na ina uzani wa tani nne unusu. Ilizinduliwa katika bustani la majengo ya bunge na inaonyesha Nelson Mandela akihimiza umoja na maridhiano.

Sanamu hiyo yenye mikono ya Mandela ikiwa wazi ilinuiwa kuonyesha Mandela alivyoliungaisha taifa zima kwa mapenzi yake.

Familia ya Madiba , viongozi wa ANC , viongozi wa Afrika na maafisa wengine wakuu walihudhuria mazishi hayo katika kijiji cha Qunu mkoani Cape Mashariki.

Mandela anakumbukwa kwa juhudi zake za kupatanisha wananchi na kupigia debe msamaha miongoni mwa watu na ndio maana leo ikawa siku iliyotengwa kwa ajili ya uzinduzi wa sanamu hiyo.

Wakati wa utawala wa wazungu, terehe 16 Disemba ilijulikana kama siku ya kuwakumbuka mashujaa wa Afrikaners walioshinda vita dhidi ya jeshi la Zulu mwaka 1883.

Zaidi ya karne moja baadaye mwaka 1961, Mandela alizindua jeshi lake la Umkhonto we Sizwe kupigana dhidi ya utawala wa wazungu.

Kuanzishwa kwa jeshi hilo la wazalendo chni ya uongozi wa Mandela kuliongeza hasira ya wazungu kumsaka na hatimaye kumkamata na kumhukumu kifungo cha maisha jela kwa kosa la uhaini


 
Shukrani kwa : Harold Dickson | Prosper Kwigize | 0752490120
Copyright © 2013. KWIGIZE NEWS AND COMMUNICATION - Haki zote zimeifadhiwa
Email us: kwigizenews@gmail.com
0764243377